Na mwandishi wetu, Kondoa
Uingizaji
wa mifugo kwenye pori la akiba la Mkungunero lililoko wilayani Kondoa
mkoani Dodoma umeathiri uhifadhi wa pori hilo na kusababisha kukauka kwa
baadhi ya vyanzo vya maji na kutoweka kwa baadhi ya wanyamapori adimu.
Meneja
wa Pori la akiba la Mkungunero, Emmanuel Bilaso akizungumza na a
waandishi wa habari waliotembelea pori hilo hivi karibuni amesema pori
hilo linalopakana na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire lina vyanzo muhimu
vya maji ambayo yanayotegemewa na wananchi wengi kwa shughuli za kijamii
na kiuchumi.
Bilaso
amesema pori hilo la Mkungunero pia lina vyanzo vya maji ya mto
Tarangire ambao ndiyo uhai wa Hifadhi ya taifa ya Tarangire na akatoa
wito kwa wananchi kutilia mkazo uhifadhi ambao una umuhimu mkubwa kwa
jamii na maendeleo ya taifa.
Amesema
operesheni inayoendelea katika pori hilo imefanikisha kukamata kwa
mifugo mingi katika pori hilo ambayo inachunga humo kinyume na sheria ya
uhifadhi ambayo inakataza shughuli za binadamu kwenye maeneo
yaliyohifadhiwa.
“Tumekamata
ng’ombe zaidi ya 230 ambao waliingizwa na wananchi kinyume cha sheria
na wamefikishwa mahakamani na kutozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni
6” alisema bwana Bilaso.
Aliongeza
kuwa kuingiza ng’ombe ndani ya hifadhi ni kinyume cha sheria ya
uhifadhi ambayo inatoa adhabu kali ikiwemo kutaifisha mifugo
inayokamatwa ili iwe fundisho kwa watu wanaovunja sheria za uhifadhi.
Nae
Mkuu wa mkoa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota amewaonya wananchi
wanaingiza mifugo katika pori hilo kuacha mara moja vinginevyo hatua
kali zitachukuliwa dhidi yao ili iwe fundisho kwa watu wanaovunja sheria
na kuingiza mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.
Amesema
wilaya inaandaa mkakati wa uwepo wa makao makuu ya ncho Dodoma na
kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Dodoma mpaka Babati
kuwa fursa ya kiuchumi kwa wananchi na taifa.
“Tuna
vivutio vingi vya utalii likiwemo pori la akiba la Mkungunero na
mapango yenye michoro ya kale, ni matarajio yetu kwamba viongozi wengi
na wabunge watapata fursa ya kutembelea na hasa kwa sasa ambapo barabara
ya lami kutoka Dodoma mpaka Babati imekamilika´alisema mkuu wa wilaya.
lenye
wanyamapori wengi wakiwemo simba, tembo, nyati na mimea adimu meneja wa
pori la akiba la mkungunero emmanuel bilaso amesema watuhumiwa
waliokamatwa
Nao
baadhi ya wananchi wanaoishi kwenye vijiji kuzunguka pori hilo
wameiomba serikali kuweka vipaumbele katika uhifadhi wa pori hilo la
akiba la Mkungunero ikiwemo kulipa fidia kwa baadhi ya wananchi
wanaotakiwa kupisha uhifadhi endelevu wa pori kama tathimini
ilivyofanywa na serikali kwa mujibu wa sheria.
Diwani
wa kata ya Itaswi Said Mohamed Chobu alisema wananchi wanatambua
umuhimu wa pori hilo lakini ni vizuri sasa wizara ya maliasili na utalii
ikalipa fidia kwa wananchi kwenye vijiji kandokando ya hifadhi ili
kuepuka uharibifu wa mazingira na migogoro baina ya wananchi na
wahifadhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni