Mwili Mwingine Waonekana Ukielea Ajali Mv Nyerere tanzia



Mwili mmoja wa mtoto umepatikana saa nne asubuhi hii, wakati wazamiaji wakiweka sehemu ya chini Maputo (boya) yanayojazwa upepo ili kukiinua kivuko cha MV Nyerere, eneo la Bwisya kisiwani Ukara, jijini Mwanza.
Kazi ya kukinyanyua kivuko hicho  kilichozama Alhamisi iliyopita na kusababisha vifo vya watu  225 ilianza jana  Jumamosi Septemba 23.
Kazi hiyo inafanywa na kampuni ya Songoro Marine chini ya usimamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Kijiji cha Bwisya Kisiwa cha Ukara kilipozama kivuko hicho, mtaalamu kutoka kampuni hiyo, Meja Songoro alisema hatua ya kwanza itakuwa kuingiza hewa ndani ya kivuko ili kuyatawanya maji na kuanza kukivuta.
“Kivuko kinaendelea kuelea kwa sababu kuna hewa ndani yake. Wakati kinageuka (kupinduka) kilichota maji, tutaanza kuingiza hewa kutoa maji na kuanza kukivuta. Tutakapoanza kuyatawanya maji hayo, pia tutapeleka boya na hii itafanya chombo kizidi kuja juu. Baada ya hapo tutakisogeza taratibu hadi kwenye maji mafupi.”
 
Usisahau Kuinstall  Andoid Applicatuion yetu ili kupata habari zetu kwa haraka zaidi. Ingia Playstore, search Manyara leo blog

Breaking: Shaffih Dauda afikishwa mahakamani... Aachiwa kwa Dhamana

Wamilikiwa wa blog ya Dauda.com  wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Mkazi Kisutu ambao ni pamoja na mtangazaji wa Clouds fm Shaffih Dauda. Wawili hao wanatuhimiwa kwa kosa la kuendesha blogs bila kuwa na kibali.

Licha ya Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 8 mwezi wa kumi,washtakiwa hao walikataa tuhuma hizo za kumiliki blog bila kuwa na kibali.
Wakili wa upande wa Jamhuri ameiomba Mahakama kuhairisha shauri hilo mpaka pale upelelezi utakapokamilika, na kwa Wakili wa upande wa utetezi Jebra Kambone ameiomba Mahakama kuwapa dhamana wateja wake kwa kuwa haki ya kupata dhamana ipo na Hakimu wa kesi hiyo amekubali kuwapa dhamana washtakiwa hao.

Shafiih na wenzake ambaye anashikiliwa ni Ben Ali (Ben On Air) ambaye alikuwa muendeshaji wa Dauda TV kupitia mtandao wa (Youtube) walikamatwa wiki iliyopita kwa kosa la kuendesha blog hiyo bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Mawasiliano ya simu kuvifikia Vijiji vyote nchini kwa gharama nafuu


Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote imejipanga kuhakikisha vijiji vyote nchinivinapata huduma ya Mawasiliano ya simu za Mkononi kwa gharama Nafuu ifikapo mwakanin,2019.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha  katika mkutano wa siku mbili wa Taasisi za udhibiti waMawasiliano katika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki(EACO),Naibu waziri wa Uchukuzi na MawasilianoMhandisi Atashasta Nditie.

Amesema hadi sasa Tanzania ina asilimia 94 ya wananchi  wanaotumia mawasiliano ya Simu za Mkononina kwamba ifikapo mwaka 2019 watanzania wote watafikiwa na huduma hiyo ya mawasiliano ya uhakika .

''Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja watanzania wote watakuwa wamefikiwa na mawasiliano ya uhakika naNinaposema mawasiliano simaanishi Mitandao yote ya Simu iwafikie ila tunamaanisha hata mtandaommoja ukifika tayari watanzania watakuwa wamefikiwa na mfumo wa Mawasiliano "Amesema Naibu waziri

Katika hatua nyingine Mhandisi Nditie Amesema mfuko wa mawasiliano kwa wote utajenga Minara yamawasiliano kwa vijiji 369 kuanzia mwezi ujao wa kumi ,hivyo kuongeza huduma ya mawasiliano,jambolitakalosaidia kuimarisha uchumi kupitia sekta ya mawasiliano.

Awali  katibu Mtendaji wa  taasisi  ya mawasiliano ya Afrika Mashariki (EACO),Ally Simba amesema.nchi zajumuia ya Afrika Mashariki zimepiga hatua kubwa katika mawasiliano ya Simu za Mkononi kwa asilimia 50na Intaneti asilimia75 ikiwemo  Tanzania yenye asilimia 94,Kenya asilimia 90 na Uganda ni asilimia 70.

Lengo la mkutano huo ni kuhakikisha vijiji vyote vilivyoko katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki visivyona Mawasiliano vinapata huduma hiyo  "Amesema

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano NchiniTCRA),Mhandisi James  Kilaba Amesema Mamlakahiyo itaendelea kudhibiti maudhui ya mawasiliano  pamoja na kusimamia  sheria ya mtandaoni

"Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kwa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki kwa kuanzisha mfuko maalamukwa ajili ya kupeleka huduma ya mawasiliano kwenye vijiji ambavyo kampuni za Simu zinaona havina mvutowa kibiasharaAmesema

Amesema mamlaka ya mawasiliano nchini imelazimika kuuza kwa mnada Masafa ya mwendo kasi ilikuwawezesha wananchi kote nchini kupata huduma ya Mawasiliano ya uhakika.
 
Mkurugenzi wa TCRA James Kilaba

WALIOKAIDI KUHAMA KWENYE MAENEO YENYE MAFURIKO SAME SASA KUKAMATWA


Eneo la Kitongoji cha Mferejini lililotengwa na Serikali kwa ajili ya kuanzisha kambi kwa ajili ya Wahanga wa Mafuriko .
Add caption
Wahanga wa Mafuriko wakianza ujenzi wa nyumba za Miti kwa ajili ya kujisitiri katika eneo la Ruvu Mferejini.
Makazi ya wananchi hawa kwa sasa wanalala nje ,wakiteseka na Baridi,Mbu na wanyama wakali kama Nyoka hali ambayo inatishia Afya zao.
Hata hivyo tayari serikali imeanza kufikisha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo ya Maji kwa ajili ya kunywa pamoja na kupikia.
 Na hizi ndio sehemu za makazi ya wananchi hawa.
Huduma Muhimu kama Choo zimeanza kujengwa katika eneo hilo.
Wananchi Jamii ya Massai pia ni miongoni mwa waathirika wa Mafuriko hayo.
Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule akiwa ameongozana  na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour wakitembelea moja ya Kaya ya Jamii ya Wafugaji walioanza maisha mapya katika maeneo yaliyotengwa na Serikali.
Baadhi ya Nyumba za Jamii ya Kimasai zikianza kujengwa katika eneo hilo.
Kama ilivyo ada kwa tamaduni za Mila za jamii ya Maasai kina mama ndio watendaji wakubwa wa shughuli za Nyumbani kiwemo ujenzi wa Nyumba kama anavyoonekana Bibi huyu.
Arikadharika shughuli ya uchotji wa maji vivyo hivyo.
 Na hii ni Familia moja ya Fashet Kimotong wakiwa katika eneo jipya  baada ya kuhama makazi yao ya wali kufuatiwa Nyumba zao kuzingirwa na maji .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

SERIKALI imetoa siku mbili kwa wananchi waliosalia katika Vijiji vya Ruvu Mferejini na Ruvu Marwa wilayani Same ,Mkoani Kilimanjaro vilivyozingirwa na maji kuondoka mara moja na kwamba watakao kaidi wataondolewa kwa kutumia nguvu na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Zaidi ya watu wapatao 2000 wamelazimika kuyahama makazi yao baada ya kufikwa mafuriko kutokana na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha huku eneo lililoathirika zaidi na mvua hizo ni ukanda wa tambarare wa wilaya ya Same unaopakana na Bwawa la Nyumba ya Mungu.

Licha ya Idadi hiyo ya watu kuyahama makazi yao lakini bado wapo waliokaidi kuondokana na hapa Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Same ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya hiyo ,Rosemerry Senyamule ,ikatoa agizo.

Serikali imetenga maeneo kando ya milima iliyopo katika kitongoji cha Mferejini kwa ajili ya Kambi za Muda kwa watu waliokosa Makazi ,Clouds Habari imefika katika Kambi hizo na kujionea maisha mapya ya wahanga wa mafuriko huku misaada ya kibinadamu ikihitajika zaidi .

Licha ya kukosekana kwa baadhi ya huduma katika eneo hili bado wananchi hawa wanahitaji msaada wa hali na mali ili angalau kuweza kunusuru Maisha yao kutokana na Baridi kali ,Mbu na hata wanyama wakali wakiwemo Nyoka.

Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi ,Aisha Amour ni miongoni mwa baadhi ya viongozi waliowatembelea wahanga wa mafuriko kwa ajili ya kutoa pole . 

Mafuriko katika vijiji hivi yanatajwa kuwa hutokea kila baada ya Miaka 10 na kwamba mara ya mwisho yalitokea mwaka 2008 huku chanzo kikitajwa kuwa ni kujaa kwa Bwawa la Nyumba ya Mungu ambapo ujazo ulifikia Mita za ujazo 689.88 ambazo kwa sasa zimeanza kupungua hadi kufikia mita za ujazo 689.80 baada ya maji kuanza kuelekea kwenye maeneo ya makazi kwa kupitia mto Pangani.

Mwisho