DC MTATURU AKEMEA VIASHIRIA VYA MGOGO WA WAKULIA NA WAFUGAJI

Na Mathias Canal, Singida 
 

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekemea vikali viashiria vya mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo ya malisho na mashamba vinavyoanza kuchipuka na kuibua hisia za sintofahamu.

Migogoro ya wakulima na wafugaji huanza kwa majibizano ya mara kwa mara kati ya wananchi wenyewe kwa kuingiliana katika maeneo yao jambo ambalo likipuuzwa ingali dogo hukomaa na kupelekea serikali kutumia nguvu nyingi katika kulimaliza.

Akizungumza na wakulima na wafugaji kwenye ziara ya kikazi katika vijiji korofi vinavyochagiza mgogoro huo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliwataka wananchi kuacha haraka kuibua hasira baina yao jambo ambalo linawezekana kutatulika.

Aliwataka wakulima ambao wamevamia katika maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya mpango wa matumizi bora ya ardhi kuondoka haraka katika maeneo hayo na kutafuta maeneo mengine kwa ajili ya kilimo kwani endapo kama watakiuka maelekezo hayo serikali itachukua hatua dhidi yao.

Aliwataka wakulima hao waliovamia maeneo hayo kufika ofisi ya Afisa Mtendaji wa kijiji ili kubaini kama wanastahili kupatiwa maeneo mengine kutokana na kukutwa katika maeneo hayo mara baada ya kuanzishwa sheria ya matumizi bora ya ardhi ya mwaka 2007.

Mhe Mtaturu alisema kuwa Mgogoro wa kimaeneo ya malisho na mashamba ambao umeanza kumea katika kipindi cha hivi karibuni Wilayani Manyoni unahusisha Vijiji jirani vya Itigi Mjini, Doroto na Damwelu vinavyochangia maeneo hayo.

Alisema kuwa ni lazima kila mwananchi kuwa wakala wa kuhifadhi na kutunza mazingira katika maneo yanayotuzunguka ikiwa ni pamoja na kutolima katika maeneo ambayo yamehifadhiwa au kupangwa kwa ajili ya mambo mengine.

Hata hivyo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi kufatilia ili kubaini aliyetoa maeneo ya wafugaji kwa wakulima ili achukuliwe hatua za kisheria kwani jambo hilo lina dalili zote za rushwa na uhujumu wa maeneo.

Sambamba na hayo pia Kaimu Mkuu huyo wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliwataka wananchi kuelekea msimu wa kulima mazao ya kipaumbele ambayo ni Pamba, Korosho, Chai, Kahawa na Tumbaku.

Aidha, alisema kuwa pamoja na mazao hayo ya kipaombele lakini wanapaswa kuongeza kasi katika kilimo cha mazao ya chakula na Biashara hususani mahindi, mtama, Dengu na zao la Alizeti.

Aidha, Mhe Mtaturu aliwashauri wafugaji kupunguza idadi ya mifugo waliyonayo kwa kuuza na kununua au kujenga nyumba za kuishi ikiwa ni njia mojawapo ya kuweza kukidhi maeneo ya malisho yaliyopo.


Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakazi wa Kijiji cha Itigi, Kata ya Itigi waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Itigi, Kata ya Itigi waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara.
Wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya serikali wakati wa Mkutano wa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu. 

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Damwelu Kata ya Ipande.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni