Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (Wa
pili kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Joseph
Nyamhanga (Kushoto) wakati alipokaribishwa katika ofisi za Wizara leo
Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt.
Leonard Chamuriho na Wa pili kushoto Katibu Mkuu Dkt. Maria Sasabo
(Sekta ya Mawasiliano).
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Kushoto),
akisalimiana na Naibu Waziri Eng. Atashasta Nditiye (Kulia), wakati
alipomtembelea Waziri Mbarawa ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Wa
pili kulia ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt Leonard Chamuriho
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa (Kulia)
akisalimiana na Naibu Waziri hiyo Mhe. Elias Kwandikwa wakati
alipomtembelea Waziri Mbarawa ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati)
akizungumza na Manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Wa
pili kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa (Wa tatu kulia), wakati
walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye
(aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), mara baada ya
kuapishwa Jijini Dar es Salaam leo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye
(aliyesimama) akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), leo Jijini Dar es
Salaam kabla ya kikao kazi na Makatibu Wakuu wa wizara na baadhi ya
Watendaji waliopo jiji Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa (Kulia)
akiwakabidhi manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye
(Kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa wakati (Katikati) vitabu vya bajeti ya
mwaka wa fedha 2017/18 ya Wizara hiyo kama mwongozo wa utendaji kazi
mara baada ya kuapishwa jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka
wafanyakazi wote katika sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kufanya
kazi kwa uadilifu na ushirikiano katika kuwahudumia Watanzania ili
kufikia malengo ya Wizara.
Prof.
Mbarawa ameyasema hayo jana katika mapokezi ya Manaibu Mawaziri wapya
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ofisini Jijini Dar Es Salaam baada ya
kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe
Magufuli Ikulu Dar es Salaam.
“Mimi
nafurahi sana kufanya kazi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano kwa sababu mimi na wafanyakazi tuko katika timu moja;
tunafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano. Katika kipindi cha miaka
miwili tumefanikiwa kufikia malengo mbali mbali ya serikali mfano ujenzi
wa reli ya kisasa na barabara “ Mhe. Mbarawa amesema.
Akiwakaribisha
Manaibu Mawaziri hao katika Wizara hiyo Prof. Mbarawa amesema yeye
pamoja na wafanyakazi wote wa wizara wamefurahi kupata mawaziri wapya
ambao watafanya nao kazi kwa pamoja katika wizara hiyo.
“Sisi
kama viongozi tunapaswa kuwa mfano katika utendaji wetu wa kazi ili
kujenga imani na umoja na wafanyakazi wetu. Tunapaswa kufanya kazi kwa
uadilifu, ushirikiano na umoja kwani haya ndio masuala ya msingi katika
utendaji kazi,” Prof. Mbarawa amesema .
Waziri
amesema Wizara hiyo imefanya kazi nzuri na hili limewezekana kwa sababu
sisi kama wizara tumezingatia maadili ya msingi katika utendaji wa kazi
zetu, kuna timu nzuri ya watalaam ambao ni wachapa kazi, wana moyo wa
kujituma na kazi zote walizozifanya zina matokeo mazuri.
Kazi
nzuri imefanyika, nawaomba waheshimiwa manaibu mawaziri tufanye kazi
kama timu moja na watalaam wetu ili tuweze kufikia malengo ambayo
tumejiwekea katika wizara yetu, amesisitiza Waziri Mbarawa.Kwa
upande wake Naibu Waziri anayeshughulikia Eng. Atashasta Nditiye
anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano amesema kuwa
amejipanga kufanya kazi na kulete matokea chanya na kwa maendeleo ya
nchi.
“Nipo
tayari kufanya kazi itakayoleta mabadiliko, tutaboresha miundombinu ili
kuchochea kasi ya ukuaji wa viwanda na kila nitakachofanya ni
utekelezaji wa yale amabayo Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli
anayatarajia,” amesema mhandisi Nditiye.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt
John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri tangu
serikali yake iingie madarakani Novemba 2015.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni