WANANCHI MATUI WALILIA HUDUMA YA MAJI SALAMA


Na Mahmoud Ahmad Matui
Wananchi wa Mji Mdogo wa Matui wilayani Kiteto mkoani Manyara wameimba serikali kuwasaidia kuweza kupata huduma bora ya Maji kwani kwasasa wanatumia maji ya vidimbwi ambayo si salama kwa afya na inahatarisha kuweza kupata magonjwa ya milipuko.
Wakizungumza na wanahabari waliotembelea mji mdogo wa Matui mmoja ya Wananchi hao Nassoro Kijaji alisema kuwa shida ya maji ndani ya mji huo imekuwa tatizo kwa mda mrefu na ahadi za kuletewa mpaka leo imekuwa historia kwetu.
Kijaji alisema kuwa wanatembea umbali wa kilimote zaidi ya kumi kufika eneo la vindimbwi ilikuweza kupata maji yaliovunwa na watu ambapo wale waliovuna maji ya mvua na kuyaweka kwenye simtanki huuza kwa takribani tsh 200 hadi 500 kwa ndoo hivyo kuwawiya vigumu wakati huu wa kiangazi kuacha shughuli za maendeleo kutafuta huduma hiyo.
“Tunaiomba serikali ya Dkta Magufuli kutuwezesha kupata huduma ya maji ilituweze kujiletea maendeleo kwa haraka badala ya sasa kuziacha shughuli zetu kwenda kutafuta maji umbali mrefu”
Nae mkazi wa Eneo la Chapakazi Hadija Imran alisema kuwa wamekuwa wakidamka usiku mrefu kuanzia majira ya saa 10 kwenda umbali wa kilometa zaidi ya kumi na kuisihi serikali kutekeleza ahadi yao ya kumtua mama ndo kwa kuwapelekea huduma ya maji hata ya visima virefu katika eneo lao.
Alisema kipato kikubwa cha wananchi wa huko ni kilimo na ufugaji ambao kwa kipindi hichi cha kiangazi wamekuwa wakitaabika kuacha shughuli hizo na kwenda kutafuta maji ya kuweza kuwasaidia hivyo maendeleo kusimama.
Aidha diwani wa Kata hiyo ya Matui Kidawa Athman alisema kuwa suala hilo amekuwa akiliwasilisha kwenye vikao vya baraza la madiwani la halmashauri ya Kiteto ambapo wameahidi kulishughuliki suala hilo japo ni mda mrefu umepita tangia suala hilo kuwasilishwa kwenye baraza hilo.
Athman alisema kuwa juhudi zinaendelea kuweza kuhakikisha wananchi wake wanaondokana na adha hiyo licha ya serikali kwa awamu iliyopita kuahidi kuhakikisha inatatua kero hiyo kwa wakati lakini hadi sasa hakuna kilichoendele ila anaamini kwa serikali hii ya wamu ya tano suala hilo litakuwa historia kwao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni