Nyota wa Liverpool Mohamed Salah
ameipelekea nchi yake ya Misri katika fainali za kombe la dunia
Urusi, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1990 baada ya kufunga goli
la penati katika dakika ya 95.
Zikiwa zimebakia dakika za lala
salama Salah alijitokeza kuipiga penati muhimu dhidi ya Congo, na
kuibua shamrashamra za nguvu katika dimba la Borg El Arab huko
Alexandria baada ya kufunga.
Sherehe za kutinga fainali za kombe
la dunia zilitapakaa mitaani, huku Jijini cairo helkopta za jeshi
zikidondosha bendera kwa maelfu ya mashabiki waliokusanyika katika
eneo la Tahrir square.
Mohamed Salah akishangilia baada ya kufunga goli la penati katika dakika za mwisho
Mashabiki wa Misri wakiwa mitaani kushangilia kutinga fainali za kombe la dunia
Nifuraha tupu jana usiku Misri baada ya kufuzu michuano ya kombe la dunia itakayofanyika Urusi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni