Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kufanya mazungumzo na ugeni kutoka Taasisi inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya Tabia ya Nchini Dunia (C40 CITIES) ofisi kwake Karimjee,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen.
Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaa Isaya Mwita ,kushoto Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati akiwa pamoja na ugeni kutoka Taasisi inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya Tabia ya Nchini Dunia (C40 CITIES) wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko.
Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen akizungumza wandishi wa habari leo mara baada ya kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita aliyesimama katikati, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko.
Picha zote na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya wa jiji.
……………
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, amesema mipango thabiti iko mbioni ili kuboresha miundombinu yenye changamoto dhidi ya mafuriko na majanga mbalimbali yanayoweza kulikumba jiji hilo.
Meya Mwita aliyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na ugeni kutoka taasisi inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya tabianchi duniani (C40 CITIES) ofisini kwake Karimjee jijini hapa.
Ugeni huo uliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa C40 CITIES Kanda ya Afrika, Hastings Chikoko na Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote duniani kutoka London, Uingereza.
Amefafanua kuwa katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuleta mtalaamu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi ambaye atafanya kazi ya kushughulikia changamoto mbalimbali zinazohusiana na masuala ya mabadiliko hayo jijini hapa.
Amesema pia wameahidi kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha maeneo ambayo yanakumbwa na mafuriko mara kwa mara likiwemo bonde la Mto Msimbazi, Jangwani na maeneo mengine.
“Leo nimekutana na marafiki zetu hawa wa C40 CITIES, tumeongea mambo mengi ya kujenga na kuliletea jiji letu maendeleo katika sekta ya miundombinu ambayo imekuwa ni changamoto katika jiji letu.
“Jiji letu linakua kwa kasi kubwa, tunatakiwa kujipanga mapema, maeneo mengi yanakumbwa na mafuriko wakati wa mvua, wananchi wetu wanahangaika, sasa imefika kipindi ambacho tunapaswa kulipatia ufumbuzi jambo hili,” amesema Meya Mwita.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa C40 CITIES, Hastings Chikoko, amesema kuwa wamekuja jijini hapa kwa ajili ya kusaidiana katika maeneo matatu ambayo ni usafiri jijini, kukabili mafuriko na ukame ili kuwezesha kilimo cha mijini.
Alisema taasisi hiyo itatoa mtaalamu/mshauri mmoja ambaye atafanya kazi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa muda wa miaka mitatu ili kutoa mapendekezo ya namna watakavyokabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ili jiji liwe salama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni