Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar viongozi watakaochaguliwa kupitia Uchaguzi
wa ngazi ya Wilaya ya Kaskazini “B” kichama Unguja kuwa mstari wa mbele
kukemea vikali tabia ya makundi na safu za uongozi zenye nia ya
kuhatarisha uhai wa CCM katika Wilaya hiyo.
Wito
huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma
Mabodi wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wilaya hiyo wa kuwachagua
viongozi wa nafasi mbali za ngazi hiyo huko Mahonda katika ukumbi wa
Ofisi ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema
matarajio ya CCM ni kuona viongozi wanaochaguliwa katika uchaguzi huo
wanachukia kwa vitendo uwepo wa baadhi ya makada wanaoendekeza makundi,
Safu na rushwa ndani ya chama hicho.
Dk.Mabodi
alieleza kwamba msimamo wa CCM ni kuhakikisha Katiba, kanuni na
miongozo inasimamiwa na kufuatwa ipasavyo ili kupata viongozi na makada
wenye uwezo wa kuendeleza mafanikio ndani ya chama hicho kwa miaka
mitano ijayo.
Aidha
aliwambia viongozi watakaopata nafasi ya kuchaguliwa kupitia uchaguzi
huo wahakikishe wanajenga ngome imara ya kisiasa katika wilaya hiyo
sambamba na kuwashawishi wapinzani waliomo katika Wilaya hiyo kujiunga
na CCM kwani ndio chama pekee kinachojali maslahi ya wananchi wote.
“Baada
ya kukamilika uchaguzi huu wa ndani ya chama chetu tuna jukumu jingine
la kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa Dola wa mwaka 2020 pamoja na kusimamia
Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kama
tulivyoahidi kwa wananchi.”, alisisitiza Dk. Mabodi.
Aliwasihi
makada watakaochaguliwa kuwa viongozi kushirikiana vizuri na makada
wenzao ambao hawakupata fursa ya kuchaguliwa kwa lengo la kuendeleza
misingi imara ya ukomavu wa kisiasa na Demokrasia iliyotukuka.
Hata
hivyo aliwapongeza wanachama hasa makada waliogombea nafasi mbali mbali
kwa kutofanya kampeni za fujo, vurugu na kuchafuana hali aliyosema kuwa
inaonyesha ishara njema ya kukamilika kwa uchaguzi huo bila kujitokeza
mapungufu.
Aidha
alisema chama hicho baada ya uchaguzi huo kinakusudia kutoa mafunzo ya
kuwajengea uwezo viongozi wa ngazi mbali mbali za chama hicho ili waweze
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Naibu
Katibu Mkuu huyo Dk. Mabodi aliwataka wanachi hasa wanachama wa chama
hicho kupuuza kauli zinazotolewa na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif za
kuwa ataapishwa kuwa Rais wa Zanzibar jambo ambalo haliwezi kutokea
kwani Rais halali wa Zanzibar ni Dk. Ali Mohamed Shein mpaka mwaka 2020.
Katika
uchaguzi huo nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti wa Wilaya , Katibu wa
Siasa na Uenezi, nafasi ya mkutano Mkuu wa Mkoa , nafasi ya Mkutano Mkuu
wa taifa pamoja na nafasi ya Halmashauri kuu ya CCM Wilaya.
-Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akifungua Mkutano
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" huko Mahonda katika ukumbi wa CCM Mkoa
wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo.
Baadhi
ya Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" wakifuatilia kwa
makini hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Dk. Mabodi huko
Mahonda.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano huo Balozi
Seif Ali Idd akipiga kura katika uchaguzi wa CCM ngazi ya Wilaya ya
Kaskazini "B" uliofanyika leo huko Mahonda katika ukumbi wa CCM Mkoa wa
Kaskazini Unguja uliofanyika leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni