WAANDISHI WA HABARI WAMETAKIWA KUIBUA HABARI ZA VIJIJINI

 Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini mkoani Morogoro ,Semina hiyo imeratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC)
Mwezeshaji wa semina Joe Nakajumo akifundisha katika mafunzo hayo leo Mkoani Morogoro
Kushoto ni Noria Damian ,katikati Editha Carlo pamoja Happines Mtweve wakifatilia mafunzo hayo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini wakifatilia mafunzo hayo kwa ukaribu
Amon Mtega kutoka Ruvuma Press club akiachangia mada katika mafunzo hayo ,kulia ni Queen Isack kutoka Kilimanjaro Press Club
Kushoto ni mwakilishi kutoka Arusha Press club Pamela Mollel,katikati ni Adam Juma kutoka Mtwara Press Club wakifatilia mafunzo
Mwandishi wa habari Laudence Simkonda kutoka Mbeya kulia Oscar Simon kutoka Rukwa wakifatilia mafunzo hayo
                                                                                            Na Pamela Mollel,Morogoro 

Waandishi hapa nchini wametakiwa kuongeza muamko katika kuandika na kutangaza habari za vijijini kwa kuwa asilimia 75ya wananchi wa Tanzania wanaishi vijijini ambako wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali
Rai hiyo ilitolewa leo Mkoani Morogoro na mwenzeshaji Joe Nakajumo katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini iliyowakutanisha wanahabari kutoka mikoa mbalimbali iliyoratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC)
Nakajumo alisema kuwa waandishi wa habari wanajukumu kubwa la kuwa karibu na jamii ya vijijini kwa kutambua shughuli zao wanazozifanya na kuzifatilia kwa kuona mafanikio yao pamoja na kuibua kero zinazowakabili
 

“Asilimia 75 ya wananchi wanaishi vijijini wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli za kilimo,ufugaji ,uvuvi,ujasiriamali hivyo ni muhimu sana kuwapa kipaumbela wananchi hawa”alisema Nakajumo
Aidha alisema kuwa moja ya majukumu ya msingi ya mwandishi wa habari ni kusaidia na kushiriki katika ujenzi wa taifa hivyo anapaswa kuudhihirishia umma kwa watu wote nchini wanapaswa kupata habari
Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo Adam Juma alisema kuwa mafunzo haya yatasaidia kuibua changamoto vijijini ambako panaoneka kusaulika kwa huduma mbalimbali za kijamii
 

Pia aliwaomba waandaji wa semina hii UTPC kuendeleza mafunzo haya kwa waandishi wa habari ili kuweza kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya taaluma hiyo
Umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC)imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa waandishi wa habari lengo ikiwa kuwaongezea ujuzi wa kufanya kazi zao kwa kufata misingi ya taaluma .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni