MKAZI WA KATA NA KIJIJI CHA BUKONDO WILAYANI GEITA AMEFARIKI BAADA YA KUSHAMBULIWA NA MAMBA



Ramadhan
Dadila ni moja kati ya watu ambao walikuwa na marehemu hapa anazungumza na waandishi wa habari namna ambavyo waliachana  wakati wakiwa kwenye shughuli za uvuvi.


Afisa mtendaji wa Kijiji hicho Bw,Beatus Mazezele akielezea namna ambavyo walipatiwa taarifa ya mtu huyo kushambuliwa na mamba .

Wanakijiji wakiwa wamekusanyika kando kando ya vikwe wakisubilia kuanza kumuwinda Mamba .

PICHA NA JOEL MADUKA. 




Mkazi   wa Kata   na kijiji cha  Bukondo
Wilayani Geita  Bw  Yusufu Samson
amemezwa  na mamba wakati  akiwa katika
shughuli  zake  za uvuvi
Oktoba  2.



Maduka Online  imefika
Kijijini Hapo na kuzungumza na Baadhi ya
watu ambao alikuwa nao katika shughuli hiyo  ya uvuvi ambapo  wameelezea
hali  ilivyokuwa na  hadi
umauti  ulipomkuta,  John Katamla
na Ramadhan Dadila,wameelezea kuwa
walikuwa  naye  wakati
wa shughuli  za  kuloa
samaki lakini hata hivyo hali haikuwa
nzuri  hivyo  ilibidi
wakunje ndoano kwa  ajili ya
kurudi Nyumbani ingawa  marehemu  alikuwa
anaendelea  kuvuta  kamba
za  nanga.

Mwenyekiti  wa
Kijiji  hicho   MAKOYE
SOJINGWANONI   amethibitisha
kutokea  kwa tukio hilo ambapo  amesema
asubuhi wamemwona mamba huyo akitembea maeneo hayo lakini  hawakuweza
kumfanya lolote  hivyo wameomba
msaada  kutoka  kwa
mali asili.


Mtendaji wa Kijiji cha Nyansalala,Bw Beatus Mazezele  amesema
tukio la kukamatwa na mamba mtu sio la mara ya  kwanza kwani yamekuwa ya kijirudia mara kwa
mara   hata hivyo ametoa wito kwa
wananchi kuachana na dhana ya kuendelea kuogelea  maeneo
ya  ziwani.




Afisa
wanyamapori  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Geita Msese  Msese amesema
hadi kufikia  siku  ya jana walipata baadhi ya vipade vya mwili
na  bado wanaendelea na jitihada ya
kuutafuta mwili huo pamoja na mamba
ambaye amekuwa ni tishio kwa wananchi wa maeneo hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni