JAMII YAASWA WAWE WEPESI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO

Na Mahmoud Ahmad Kiteto
Jamii mji mdogo wa Matui wilayani kiteto imeaswa wawe wepesi katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo zitakazosaidia ukuaji wa maendeleo na hivyo kuweza kupata huduma muhimu kwa jamii hiyo.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata ya Matui Kidawa Athman Iyavu wakati akiongea na wanahabari waliotembelea kata hiyo kujionea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na halmashauri pamoja na nguvu za wananchi.
Alisema kuwa ilikufikia malengo ya mji mdogo lazima wananchi na viongozi wakafanyakazi kwa ushirikiano utakaosaidia kumaliza miradi kwa wakati ikiwemo mradi wa wodi pacha za kinamama,watoto na Chumba cha upasuaji ili kuweza kupata hadhi ya kituo cha afya.
“Nawasihi wananchi wangu hapa matui tuwe wepesi katika kuchangia maendeleo yetu tukisaidiana na serikali kuhakikisha tunafikia kwenye mafanikio ya upataji wa huduma bora za Afya bila kutembea umbali mrefu” asisitiza Iyavu
Nae Mtendaji kata ya Matui Zainab Mahiza alisema kuwa mradi huo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha milioni 100 na hadi sasa zimetumika kiasi cha million 37 ambapo halmashauri imechangia milioni 23 na wanachi wamechangia milioni14.5 ambapo mpaka sasa wodi mmoja imepauliwa na wanasubiria fedha za ujenzi wa awamu ya pili.
Alisema kuwa kutokana na ukosefu wa fedha mradi huo haujakamilika kwani jamii yetu inategemea kilimo kujipatia riziki na fedha na msimu huu haukuwa mzuri hata shughuli za maendeleo zimekwama kutokana na hali hiyo.
“Nawasihi wananchi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa chakula hicho kidogo mkitunze ilikiweze kuwasaidia kuendesha maisha pia wafugaji wenye mifugo wauze michache kuwezesha kununua chakula kwa akiba yao” alisema Mahiza

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni