Ahmad
Mahmoud
Mwaka huu
Namshukuru mungu kunijaalia kuweza kutembelea maeneo ya vijijini ikiwa ni
katika kutekeleza majukumu yangu ya utafiti wa habari kwa jamii zilizopo pembezoni
na kuchaguwa wilaya za Chemba,Kondoa Mji na Vijijini.
Suala la
kutembelea maeneo hayo ni kufanya utafiti wa kihabari ambao utasaidia kuibua
kero mbali mbali wanazokutana nazo wananchi na kujua miradi ya maendeleo ambayo
serikali imetekeleza sahemu hizo,za pembezoni mwa jamii hususani vijijini.
Kumekuwa na
Changamoto kubwa ndani ya wilaya hizo kiasi kunatakiwa juhudi za mara kwa mara
kwa waandishi kufika huko, ambapo waandishi wengi ni nadra sana kufika maeneo
ya vijijini sio Kondoa pekee na maeneo mengine hapa nchini kusaidia kuibua
matatizo na juhudi za serikali kuatatua kero zao,
Hapa
nawashukuru sana Muungano wa klabu za Waandishi wa Habari hapa nchini(UTPC) kwa kuja na mpango wa mafuzo ya wandishi wa
habari za vijijini hii naona ni wakati muafaka na msingi wa kuweza kuwasidia
wananchi kuziunganisha na mamlaka zao kuweza kuibua kero zao, japo mimi sio
mmojawapo niliepata mafunzo hayo ila natekeleza wajibu.
Mwezi wa 3
mwaka huu tarehe 8 nikiwa mkoani Arusha ambapo ni kituo changu cha kazi Napata simu
ikiniomba kwenda kondoa kwenye tukio la Kampuni ya madini ya Kondoa Minning na Kikundi
cha wachimbaji wadogo wa madini ya Dhahabu(KUMUCHA) kwenye Kijiji cha Changaa.
Nilifika
kondoa majiba ya saa 7 mchana kwa basi la kampuni ya Champion na kupokelewa na
wenyeji wangu viongozi wa kikundi cha kumucha na mara moja kuelekea maeneo ya
Mtaa wa Tumbelo ambapo yapo machimbo wanaogombea na kampuni ya Kondoa Minning T
Ltd kwa mda mrefu sasa bila kupatiwa ufumbuzi wa suala hilo ambapo mamlaka hadi
sasa zipo kimya kutoa tafsiri ya nani hasa mmiliki wa eneo hilo la migodi
iliyopo Changaa.
Leo
Sintazungumzia mgogoro huo ambao kwa sasa upo katika hatua za kutolewa majibu
ya kina na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kondoa Ndugu yangu Fallesy
Kibasa kwanza nampa Hongera kwa utekelezaji wa majukumu pili namwambia sheria
ifuate mkondo wake katika kuhakikisha wananchi wanyonge wanapata haki yao bila
kujali maslahi mapana ya wenye nacho.
Bila kusahau Ofisi ya madini kanda ya kati na
Afisa Madini Makazi Dodoma nao pia wapo katika mikakati hiyo ya kutatua mgogoro
huo, Japo wao ndio chanzo cha mgogoro huo kwa kushindwa kutafsiri sheria ya
madini ya mwaka2010 kwa vitendo na kuichukulia maamuzi kwa wakati ambayo
ingeondoa sintofahamu iliyopo katika ya wachimbaji na kampuni ya Kondoa Minning.
Suala
nalotaka kulizungumzia leo ni suala la kampuni za simu za mikononi ambazo zipo
hapa nchini zikiwaunganisha wananchi katika suala zima la mawasiliano ili
waweze kujiletea mendeleo yao kupitia mawasiliano ya kibiashara na hata sasa
wakati serikali inatekeleza sera ya Uchumi wa kati wa Viwanda nayo ni kiungo
muhimu wa kufikia malengo hayo.
Kumekuwepo
na sintofahamu kubwa katika suala zima la fedha za huduma ambazo makampuni ya
simu yanatakiwa kurudisha kwa wananchi na sheria zinazoyataka makampuni hayo
kuingia mkataba na vijiji kwenye maeneo ya vijiji hususani hifadhi za milima.
Na maeneo
mengi ya Vijijini viongozi wa serikali wanatakiwa kulifuatilia hilo kwenye
maeneo mengi ya vijiji kubaini mihutasari mingi walioingia viongozi wa serikali
za vijiji mingi haipo kwa maslahi ya wananchi wa kurudisha fedha za huduma na
malipo ya maeneo.
Utakuta
maeneo mengi yana migogoro ambayo kama viongozi au mwanasheria wa Halmashauri
angeshiriki katika kuandaa mchakato mzima wa miongozo ya kisheria, basi
kusingetokea matatizo kama hayo ambayo kuna vijiji Takribani 10 ndani ya wilaya
ya Kondoa ambavyo havinufaiki na fedha za huduma wala maeneo yao waliowekewa
minara ya simu za mkononi na makampuni hayo.
Sehemu
nyingine utakuta hawajalipwa Takribani miaka mitano sasa na haijulikani Fedha
zinaingia kwa nani na vijiji vimeibua miradi ya maendeleo ambapo kama fedha
hizo zingeingia kwenye vijiji hivyo ingasaidia kukuza miradi hiyo na kujikuta
vijiji vinapata maendeleo Tarajiwa ikiwemo miradi ya Afya,elimu na maji.
Hapa
ntaizungumzia moja ya Kata na Kijiji ambacho kitakuwa mfano wa vijiji hivyo 10
Thawi ni mojawapo ya vijiji hivyo na inakabiliwa na changamoto kubwa ya huduma
muhimu ya kijamii Maj,i hawa wanatumia maji ya Mto Bubu, maarufu ndani ya
wilaya hiyo, lakini changamoto kubwa wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya
mlipuko wanatumia maji hayo kuongea kufulia na mifugo humo humo kwa wakati
mmoja hii inaonyesha ni kwakiasi gani fedha hizo zingeweza kuwasaidia
kuondokana na adha hizo japo kidogo ingeondoa
Aidha kama sio Afisa wa Kampuni hiyo na
viongozi wachache kuingia makubaliano ya kinyemela kwa afisa wa Kampuni ya simu
za mkononi ya Tigo kufika na kuuhadaa uongozi na wananchi kuwa kampuni hiyo
inanunua maeneo ya kuweka minara kinyume na sera ya kampuni hiyo kukodisha kwa
wananchi aua kijiji husika, hilo ni ukiukaji
wa mkataba na kuuziwa eneo la mlima AMASASOO uliopo kijiji cha Thawi kata ya Thawi
wilayani Kondoa ,
Hii
inaonyesha ni kwa kiasi gani sheria bado nataratibu hazikutumika, na hata
viongozi walipohoji waliwaambia ntapeleka eneo lengine hivyo msukumo wa
wananchi waliokuwa wanahitaji huduma hiyo ndio uliopelekea maamuzi ya kuumuuzia
aliedai ni Afisa kutoka kampuni ya Tigo kwa makubaliano ya shilingi za kitanzania 500,000
kwa eneo la hifadhi ya mlima huo wa Amasasoo, hapa utaona jinsi misitu
inavyouzwa kinyume na sheria.
Narudia
ndugu yangu suala hilo lilifuatiliwa na mbunge wa jimbo la Kondoa kaskazini dkta.
Ashatu Kijaji ambaye pia ni Naibu waziri wa fedha na Mipango lakini hadi
naandika makala haya wananchi hao bado mnara unasumbua huduma walizotarajia
hawapati kwa uhakika jambo linalotia simanzi kama kampuni hizo zipo kwa ajili
ya kutoa huduma au zipo zipo tu.
Sijaongelea
Fedha za Huduma ambazo ni haki yao kisheria kurudishwa kwa ajili ya maendeleo
utaona ni kwa jinsi gani utaratibu huo unavyotumika kurisha maendeleo nyuma
ndani ya kijiji na hapa utaona na kujua naongelea nini katika suala zima la
makubaliano ya makampuni ya simu za mikononi
kwani nina
uzoefu wa masuala haya ndani ya ulipaji mfano upo wazi kule Salanka
nilifuatilia Fedha walizokuwa wakiidai Kampuni ya Vodacom na Airtel zilikwama
kwa mda hadi walipolipwa Stahiki yao baada ya kulifuatilia tena kwa Gharama
Hadi Dar es Salaam nikiwa na mwenyekiti wa kijiji hicho wakati huo.
Hata hivyo
ilibidi nifike kwa mwanasheria na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Kondoa
Vijijini kupata ufafanuzi kuhusiana na mbunge wa jimbo hilo alifikia wapi baada
ya kumuachia suala hilo mwanasheria wa halmashauri kulifuatilia juhudi ambazo
hadi sasa hazijapatiwa ufumbuzi wowote hadi naandika makala hii
Japo hapo awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Kondoa Vijijini Fallessy Kibassa tulitofautiana kimtazamo baada ya mimi
kuandika story kuhusiana na suala hilo na mkurugenzi huyo kuniita muungo mbele
ya Katibu mkuu wa Tamisemi Mussa Iyombe juu ya suala hilo wakati nikizungumza
nae akiwa morogoro kwa njia ya simu tena simu ya Bosi ofisini kwa katibu mkuu
Dodoma
Ilibidi nifike
kwa mwanasheria wa Halmashauri ya Kondoa Vijijini Kuulizia suala hilo na
kunieleza kuwa suala hilo wameliachia vijiji kuandaa muhtasari upya na makubaliano
mapya ilikuweza kuliendea jambo hilo na majibu yatakuwa hivi karibu kwani
juhudi zinaendelea kuhakikisha mbunge anapatiwa majibu ya suala hilo na
wananchi wanapata fedha za huduma.
“Ndugu
mwandishi hapa kuna mkanganyiko wa kisheria ila vijiji vina mamlaka yake
kisheria kuamua matumizi ya ardhi hivyo suala hili wao watakuwa na maamuzi ya
kutuletea sisi tuweze kufuatilia” aliongeza mwasheria huyo.
Utaona ni
jinsi gani huduma za simu za mikononi zilivyokuwa changamoto vijijini hususani
ambapo bado wengi wao taratibu kanuni na sheria kwao vimekuwa ni kama jua na
kiza hivyo kukuta sheria zinawapitia kando hata wakuongoza nao wanatoa majibu
ya kufikirika zaidi kuliko kisheria.
Kwa upande
mwingine nataongelea suala la Tigo pesa huku vijijini ni mwiba mchungu kuna
watu wamelizwa fedha zao na wahudumu wa kampuni ya tigo hapa namzungumzia Bi
Ziada Abdi Ally mwenye no 0711480481 aliehamishiwa Fedha kiasi cha 970 000
tokea mwezi wa nane na mfanyakazi wa idara ya mauzo ya kampuni ya Tig joseph
maginga kwenye namba zake Tofauti 0716123207 na 0710040034.
ambapo Kampuni
hiyo imekuwa ikimzungusha bila majibu
wala kumlipa fedha zake za huduma imekuwa deni, wanamwambia aende polisi nako
wanamzungusha hadi leo upelelezi haujakamilika na mtuhumiwa anadunda mitaani
hapa utaona nayo yazungumza ujue ni kiasi gani wananchi vijijini wanavyoumia.
Hiyo ni tigo
kama zitafuatiliwa na kampuni nyingine utaona mlolongo wa matukio hayo yalivyo
mengi waswahili wanasema ‘panapofoka moshi ujue moto upo karibu” huo ni msemo
wa Kiswahili na una maana kwa serikali yetu kutupia macho sio kondoa tu kwa Tanzania
nzima kwa kila aliye na dhamana kuhakikisha anawajibika sio mpaka viongozi wa
kitaifa kufika maeneo yao.
Unaweza
kusema Kondoa na Chemba zipo Kisiwani kwani kumekuwepo na matukio mengi tena ya
ubadhirifu wa miradi ya mendeleo na serikali imekuwa kimya licha ya kutakiwa
kutolea maelezo kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa huu ucheleweshaji wa majibu
na kutofika kwa wakati ndio matatizo yanakuwa makubwa na malengo ya mendeleo
yanakuwa hayajafikiwa.
Kama masuala
ya kisheria yangefuatwa na miongozo kwa viongozi wa serikali za vijiji
ingekuwepo hapa suala zima la migogoro mingi ya Ardhi na masuala ya mbalimbali yahusuyo maendeleo na migogoro isingekuwepo na ingekuwa historia naomba viongozi taasisi za kisheria
na serikali kutembelea ndani ya wilaya hizo kuwasaidia wananchi katika masuala
ya kisheria na kutoa elimu ya mausala hayo na mengine mbalimbali lengo likiwa ni kuondoa dhana ya migogoro iliyopo ambayo inafukuta chini kwa chini na serikali ndani ya wilaya ikidai imetatua migogoro 8 kati ya kumi na tatu
Endelea kunifuatilia
katika makala inayofuatia kuhusu ziara yangu kwenye wilaya hizo.
Ahmad
Mahmoud ni mwandishi wa habari Anapatika kwa No.0745159196
Email.ahmad2mahmoud@gmail.com
Mwisho………………….