Mahmoud Ahmad Arusha
…………………………………….
IDARA ya Uhamiaji mkoa wa Arusha, January 16 inawarejesha kwenye
kambi ya wakimbizi raia wa Burundi 21 ,akiwemo mwanamke
mtanzania,walionyimwa hadhi ya ukimbizi nchini Kenya..
Afisa Uhamiaji mkoa wa Arusha,
Ndelema Mwakipesile, alisema hayo ofisini kwake kuwa wakimbizi hao
akiwemo mwanamke mtanzania ambae ameolewa na raia wa Burundi,
walikataliwa kuingia nchini Kenya kutokana na kutokuwa na sifa za
ukimbizi.
Mwakipesile,alisema raia hao wa
Burundi, waliingia nchini wakipitia mpaka wa Kabanga uliopo mkoani
Kigoma na kudai wamekuja kuwatembelea ndugu zao lakini mara baada ya
kuingia nchini walibadirisha mawazo na kuamua kwenda nchini Kenya
kutafuta hifadhi kwenye kambi ya Kakuma nchini Kenya.
Raia hao 21 wakiwemo watoto 14
walipofika mpakani Namanga wakitaka kuingia nchini humo walidai
wanatafuta hifadhi ya ukimbizi na serikali ya Kenya iliwazuia na
kuwarejesha Tanzania ,ambako ndiko walikopitia kuelekea Kenya.
Mwakipesile, alisema cha
kushangaza raia hao wa Burundi kila mmoja ana hati ya kusafiria jambo
ambalo linaonyesha walikuwa wamejiandaa kwa kuwa sheria za kimataifa za
ukimbizi haziruhusu mkimbizi kuwa na hati bali mkimbizi anakuwa na vitu
vichache tu pia mkimbizi hachagui kambi ya kupelekwa .
Alisema walipoulizwa kulikoni
waende Kenya, wakimbizi wamesema kuwa wamekuwa wakiingia nchini mara kwa
mara kwenye kambi ya wakimbizi ya Kibondo,na wamekuwa wakirejeshwa kwao
mara kwa mara wanapoingia nchini.
Mwakipesile, alisema wakimbizi hao
hataki kurejeshwa kwao sasa wamebadirisha mawazo na kuamua kutafuta
hifadhi nchini Kenya ili kukwepa kurejeshwa kwao.
Alisema wanarejeshwa makwao kwa
kuwa hawana kosa lolote kwa mjuibu wa taratibu za kimataifa hivyo
watapelekwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Kibondo, ili wasubiri taratibu
zingine .
Mwakipesile alisema kulingana na
sheria mkimbizi hawezi kuomba nchi ya kwenda, pia haruhusiwi kwenda nchi
ya tatu kutoka kwao bali anatakiwa kukimbilia nchi wanayopakana nayo
Raia hao wa Burundi, walikutwa ndani ya Basi la Tahmeed Coach,
lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Nairobi nchini Kenya na
walipofika mpaka wa Namanga, wakazuiliwa kuingia nchini Kenya .
Rai mmoja wa Burundi,ambae
hakutaka jina lake liandikwe kwa sababu ya usalama ,ambae ni dereva wa
malori,amesema wamekuwa wakiingia nchini mara kwa mara kwenye kambi ya
wakimbizi na wamekuwa wakirejeshwa kwao sasa wanataka kwenda kuishi
kwenye kambi iliyo mbali na kwao kwa kuhofia usalama wao.
Alisema mwezi Desemba mwaka jana
akiwa nyumbani kwake nchini Burundi,watu watatu waliuliwa mbele ya
nyumba yake na watoto wake wamekuwa wakiogopa kuishi kutokana na
kutokuwepo amani nchini mwao na hiyo ni sababu ya msingi ya kuomba
ukimbizi.
Alisema kuwa yeye amekuwa ni
dereva wa malori kwa miaka 20 amekuwa akisafirisha mizigo kata ya
Tanzania na Burundi, lakini kutokana na ukosefu amani nchini mwao
ameamua kikimbia kutafuta hadhi ya ukimbizi nchini Kenya.
Alisema Tanzania anaipapenda
tatizo ni kuwa Tanzania imekuwa ikiwarudisha mara kwa mara nchini
Burundi hivyo wanaomba kwenda nchi ya mbali ili wasirudishwee mwakwao.
Ameongeza kuwa maafisa wa Burundi wamekuwa wakienda kwenye kambi
ya wakimbizi na kuwatambua na kasha huuliwa hivyo wanahofia usalama
wao.
Kwa upande wake Mtanzania
aliyeolewa na raia huyo wa Burundi, Eva Michael Magumula,(37) mzaliwa wa
Dodoma, alisema ana watoto 6 inalazimika aambatane na mume wake ili
waweze kulea familia yao.