EAC Deputy Secretary General (Finance and Administration), Hon. Jesca Eriyo, making her remarks during the official opening of the EAC-EU-IMF Conference on EAC integration.
Na Mahmoud
Ahmad Arusha
Jumuiya ya
Afrika mashariki,shirika la Fedha duniani(IMF)na mashirika yasio ya kiserikali
kutoka nchi za jumuiya hiyo yamekutana kujadili masuala ya mtangamano wa Soko
la pamoja na forodha ya pamoja itakayopelekea kuwa na fedha ya Pamoja ifikapo
mwaka 2024.
Akizungumza
katika mkutano huo uliokuwa ukijadili masuala ya kitakwimu yatakayopelekea kuwa
na Fedha ya pamoja ifikapo mwaka 2024 Naibu Katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Jesca Erio
alisema kuwa mkutano huo ni muhimu katika kukuza na kuendeleza jumuiya
ilikufikia malengo kusudiwa ya kuwa na fedha ya pamoja.
Erio alisema
kuwa mkutano huo wa siku mbili uliowakutanisha watunga sera magavana wa benki
kuu, wangalizi na wasimamizi wa soko,Mashirika yasio ya kiserikali na sekta
binafsi kutoka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili changamoto na mafanikio
ya soko la pamoja na ushuru wa forodha itakayopeleka kuwa na fedha ya pamoja.
Alisema
suala la takwimu za kiuchumi ni suala mtambuka linalohitajika kulifanyia kazi
na kujua ni jinsi gani unaweza kulifanikisha katika kuweza kupata na kufanikiwa
kuweza kufikia fedha ya pamoja ifikapo mwaka 2024.
“Kuwa na
Uchumi imara katika nchi wanachama itapelekea kuwa na nguvu za kiuchumi kwa
mataifa ya jumuiya yetu hivyo kuna kila sababu ya kuangalia na kujua uchumi wa
nchi moja moja itakaotufikisha kwenye malengo ya maendeleo ya kiuchumi kama
jumuiya”aliongeza Erio.
Alisema
kupata takwimu sahihi za kiuchumi hususani maeneo ya Vijijini imekuwa ni
changamoto kubwa kwa maeneo mengi ya nchi wanachama ambapo uongozaji wa
maendeleo kwa takwimu za nchi zetu katika kukuza maendeleo pia imekuwa ikiyumba
mara kwa mara.
Suala la
ukusanyaji wa mapato bado limekuwa changamoto kubwa katika kukuza uchumi wa nchi
zetu ambapo bado kumekuwa na uchelewaji wa kupata takwimu katika uzazi na vifo
na kuwa na taarifa zisizo kamili kwa nchi zetu,
“Uwekezaji
wa Elimu,Afya bado imeonekana kuwa na chnagamoto kubwa kutokana na kutokuwa na
usahihi wa kitakwimu hali inayopekea kutoweza kuwa na bajeti nzuri katika
maeneo hayo”aliongeza Erio
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni