Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akijadiliana
jambo na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba (kushoto) na
Mkurugenzi kutoka Bomba la Mafuta la TAZAMA, D. Legge (kulia).
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), na Waziri wa
Nishati wa Zambia, David Mabumba wakifurahia jambo mara baada ya
mazungumzo baina yao yaliyofanyika Ofisini kwa Waziri Muhongo jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) na Waziri wa
Nishati wa Zambia, David Mabumba (wa tatu kutoka kushoto), wakiwa katika
picha ya pamoja na Ujumbe ulioambatana na Waziri Mabumba. Wa Tatu
kutoka Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Profesa James Mdoe.
Waziri
wa Nishati wa Zambia, David Mabumba (kushoto) akimuaga Waziri wa
Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka
kushoto) baada ya kikao chao kilichofanyika ofisini kwa Waziri Muhongo.
Wa pili kutoka Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa James Mdoe
akiagana na Mkurugenzi kutoka Bomba la TAZAMA, D. Legge.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia)
akizungumza na Waziri wa Nishati wa Zambia David Mabumba (wa tatu kutoka
kulia) na Ujumbe wake, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisisitiza jambo
wakati wa kikao chake na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba na
Ujumbe wake (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es
Salaam.
Na Veronica Simba.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati wa
Zambia, David Mabumba, wamekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuboresha
Bomba la Mafuta la TAZAMA ili liweze kuwanufaisha wananchi wa Tanzania
na Zambia kama ilivyokusudiwa.
Mazungumzo
yao yaliyofanyika mapema leo, ofisini kwa Waziri Muhongo jijini Dar es
Salaam, ni kufuatia makubaliano ya marais wa nchi husika, Dk John
Magufuli na Edgar Lungu; kuhusu kuboresha zaidi Bomba la TAZAMA na Reli
ya TAZARA.
Marais
Magufuli na Lungu, walifikia makubaliano hayo jana katika mazungumzo
rasmi yaliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam ambayo ni mojawapo ya
shughuli mbalimbali zilizopangwa katika ratiba ya ziara ya siku Tatu (3)
ya Rais Lungu iliyoanza nchini Jumapili, Novemba 21 mwaka huu.
Waziri
Mabumba ambaye alifuatana na Ujumbe wa Viongozi na Maafisa waandamizi
kutoka TAZAMA na wizarani kwake; aliafiki mapendekezo yaliyotolewa na
Waziri Muhongo kuhusu namna pande hizo mbili zitakavyoshirikiana katika
utekelezaji wa agizo la Marais wao ambayo ni pamoja na wataalam wa pande
zote kukutana na kufanya majadiliano pamoja na kufanya ziara kukagua
utendaji kazi wa Bomba hilo.
Aidha, Mawaziri hao walijadiliana kuhusu namna ambavyo Zambia itanufaika na gesi asilia iliyogunduliwa Kusini mwa Tanzania.
Kikao
hicho pia, kilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Wizara ya Nishati na
Madini – Tanzania, akiwamo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa James
Mdoe.