Marekani imethibitisha kifo cha
kiongozi mwandamizi wa al-Qaeda aliyeshambuliwa na ndege
inayojiendesha yenyewe kaskazini mashariki mwa Afghanistan.
Kiongozi huyo Farouq al-Qahtani,
ambaye ni kiongozi pekee katika eneo hilo aliuwawa wiki mbili
zilizopita katika shambulizi ambalo Pentagon imesema limefanikiwa.
Al-Qahtani ambaye ni mzaliwa wa
Saudi aliwekwa kwenye orodha ya magaidi wanaotafutwa mno na Marekani
mwezi Februari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni