Na Mahmoud
Ahmad Arusha
Serikali
imetakiwa kulipa kipaumbele suala zima la Mabadiliko ya Tabia nchi ambapo
imeonekana shughuli za kibinadamu zimakuwa zikiathiri mazingira kwa sehemu
kubwa hapa nchini inayopelekea mabadiliko ya Tabianchi na ongezeko la joto.
Akitoa Mada
kwenye semina ya Waandishi wa Habari iliyoandaliwa na Oakios Tanzania
Mkurugenzi wa Taasisi ya Carbon Tanzania Jo Anderson alisema kuwa shughuli za
kibinadamu hapa nchi zimakuwa ndio sababu kubwa ya ongezeko la Joto
linalopelekea Mbadiliko ya Tabianchi.
Alisema kuwa
Maeneo mengi ya vijijini ndio yameathirika ikiwemo ukataji wa kuni na uharibifu
wa vyanzo vya maji pamoja na matumizi ya kilimo katika kubadilisha matumizi ya
misitu kwenda kwenye kilimo.
Alisema kuwa
Wandishi wa habari wamekuwa wakipata changamto kubwa kuandika habari za
kisayansi na hivyo kujikuta wakiwa hawana uelewa mkubwa kwenye masuala hayo
kitaaluma ambapo semina hiyo itawapa mwanga kuhusiana na mabadiliko ya
Tabianchi katika kuandika habari zao.
“Shughuli za
kibinadamu zimakuwa ndio changamoto kubwa ya mabadiliko ya Tabianchi ambapo
uharibifu wa mazingira kwa ukataji miti na uharibifu wa vyanzo vya maji,na
Ardhi kunakoenda sambamba na uharibifu wa misitu”alisisitiza Anderson.
Kwa upande
wake Maratibu wa semina hiyo Silvia Ceppi alisema kuwa semina hiyo ya siku moja
kwa wanahabari ni kuwapa uelewa wa masuala mazima ya kisanyansi kujua
mabadiliko ya tabianci katika kuboresha taarifa zao wanazoripoti kila siku juu
ya kadhia hiyo.
Alisema kuwa
uzalishaji wa gesi joto kunakofanywa na mataifa yenye viwanda humu duniani ndio
sababu kubwa ya uharibifu wa mazingira na kuwapa changamoto kubwa ya kuandaa
mikakati ya uthibiti wake na hivyo kuiomba serikali kutupia macho masuala ya
uharibifu wa mazingira na ongezeko la joto hapa nchini.
Mwisho……………………………………………………………
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni