Donald Trump atakuwa rais wa 45 wa
Marekani baada ya kupata ushindi wa kushtukiza dhidi ya mpinzani wake
wa chama cha Democratic Bi. Hillary Clinton.
Ushindi wa mgombea huyo wa chama cha
Republican umepatikana baada ya kuibuka na ushindi katika majimbo
yenye kura nyingi licha ya kura za maoni kuonyesha Clinton anafanya
vizuri.
Trump alikuwa anahitaji kura 270 tu
kutangazwa rais wa Marekani lakini hadi sasa amefikisha kura 288
dhidi ya 218 za Clinton.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni