VIFAA VYA KUJIKINGA NA HEWA CHAFU VYAADIMIKA DELHI NA KUIBUA HOFU

Hofu imewakumba wakazi wa Delhi nchini India kufuatia kukosekana kwa vifaa vya kujikinga na hewa chafu iliyotokana na uchafuzi mkubwa hewa katika mji mkuu huo wa India, huku vifaa hivyo vikikosekana madukani.

Wauzaji wa vifaa hivyo wamekuwa na kazi ya kutuliza hasira za wateja wao waliofurika madukani kununua vifaa hivyo vya kusaidia kuchuja hewa chafu, huku wateja wakikerwa na kungojea bidhaa hiyo kwa siku nzima.

Duka kubwa linalouza vifaa hivyo vya kujikinga na hewa chafu vya kampuni ya Vogmasks, limesema limekaukiwa kabisa na hakuna akiba iliyobakia dukani na wateja wametakiwa kungojea hadi leo mchana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni