Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo
amejifunga Real Madrid kwa kukubali kutia saini mkataba mpya
utakaomuweka kwenye klabu hiyo hadi Juni 2021.
Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa
Ureno mwenye miaka 31, mkataba wake wa sasa unaisha Juni 2018, lakini
hii leo atatia sani mkataba mpya wa miaka mitano.
Chini ya mkataba huo mpya
imeripotiwa kuwa mshahara wa wiki wa Ronaldo utabakia paundi laki
365,000. Ronaldo ameifungia Real Madrid magoli 371 tangu ajiunge nayo
mwaka 2009.
Cristiano Ronaldo akiwa amepozi na kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Real Madrid kulitwaa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni