JAJI AMUAGIZA MPENZI WA BOBBI KRISTINA BROWN KULIPA DOLA MILIONI 36


Jaji mmoja huko Atlanta amemuagiza mpenzi wa marehemu Bobbi Kristina Brown, Nick Gordon, kulipa kiasi cha dola za Marekani milioni 36 kwa kusababisha kifo chake kimakosa.

Kristina Brown, ambaye ni binti wa Whitney Houston na Bobby Brown, alikutwa akiwa amepoteza fahamu kwenye bafu, uso wake ukiwa kwenye maji Januari 2015.

Mpenzi wake Gordon, ambaye alikuwa akiishi naye pamoja na rafiki moja walikuwa katika ripoti ya polisi iliyoeleza walikuwemo nyumbani wakati wachunguzi walipofika katika eneo la tukio la kifo.
Bobby Brown akionyesha picha ya utoto ya Bobbi Kritina wakati akitoa ushahidi Mahakamani

          Bobby Brown akiwa kwenye majonzi makali wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni