Binti wa miaka 14 amekuwa Muingereza wa kwanza kuridhia mwili wake kuhifadhiwa katika mitungi maalum ya kungandisha mwili, baada ya kushinda kesi ya pingamizi lililowekwa na baba yake.
Binti huyo ambaye ni mkazi wa London, alibainika kuwa na saratani Agosti mwaka jana na kisha kufa mwezi mmoja uliopita baada ya tiba zote alizopatiwa kushindwa kumtibu.
Binti huyo alivutiwa na ahadi ya kwenye tovuti ya kampuni ya cryogenic, ambayo ilimshawishi iwapo mwili wake utagandishwa kwenye mitungi yao, siku moja itakapopatikana tiba atapa fursa ya kutibiwa na kufufuka.
Barua ya binti huyo iliyoeleza sababu ya yeye kutaka mwili wake ugandishwe kwenye mitungi ili ikipatikana tiba atibiwe na kufufuka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni