DC MWILAPWA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MAJI KUHUSU MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA



Mkuu wa wilaya ya Tangaa,Thobias Mwilapwa akifungua mkutano wa akifungua mkutano wa wadau kuhusu mkataba wa huduma kwa mteja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) uliofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na kulia ni Afisa Tarafa ,Suleiman Zumo anayefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji hiyo,Haika Ndalama
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa kikao hicho kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akimsikiliza kwa umakini 




Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa),Haika Ndalama akzingumza wakati wa kikao hicho cha wadau
Wananchi wa Jiji la Tanga wakiongozwa na madiwani wao waki fuatilia kikao hicho kwa umakini mkubwa katikati ni Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga ,Mohamed Haniu
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mustapha Selebosi akiuliza swali kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Veta mjini hapa

Diwani wa Kata ya Msambweni (CUF)Abdurahamani Hassani akiuliza swali kwenye mkutano huo
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Dorah Ilo kulia aakiteta jambo na Afisa Tarafa Suleimani Zumo wakati wa kikao hicho cha wadau
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Dorah Ilo akifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijiri kwenye kikao hicho
Kushoto ni Maafisa wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini na wananachi wakifuatilia kikao hicho wa kwanza kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Mteja wa Mamlaka hiyo,Mohamed Pima




Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akisaliana na Afisa Tarafa,Suleiman Zumo kabla ya kufungua mkutano huo katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi

Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kushoto akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga (CCM)Mustapa Selabosi kabla ya kuanza kikao hicho katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa)Haika Ndalama
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kushoto akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kikao hicho. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

MJAMZITO JANET JACKSON AFANYA MANUNUZI JIJINI LONDON

Mwanamuziki Janet Jackson ambaye ni mjamzito kwa sasa ameonekana akiwa anafanya manunuzi Jijini London mapema wiki hii.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 50 anatarajia kupata mtoto na mumewe Wissam Al Mana, alionekana akifanya manunuzi katika duka la Back In Action Jijini London.


Janet dressed alikuwa amevalia juu fulana na chini suruali pana ya traksuti alionekana akiwa bado na mvuto na muonekano mzuri licha ya kutopaka vipodozi.
                      Mwanamuziki Janet Jackson akitoka ndani ya duka la bidhaa Jijini London
            Janet Jackson akiingia kwenye gari alilotumia kwenda kufanya manunuzi 
         Janet Jackson akiwa na mumewe Wissam Al Mana picha hii walipiga Oktoba 2010

MAZOEZI YA SERENGETI BOYS KABLA YA KUVAANA NA VIJANA WA CONGO JUMAPILI

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, wakijifua kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
Kocha wa Makipa wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Muharami Mohammed maarufu kwa jina la Shilton (wa pili kushoto) akiwanoa vijana wake, Kelvin Kayego (kushoto), Ramadhani Kabwili (wa tatu kushoto) na Samwel Brazio kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
Madaktari wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Dk. Sheicky Mngazija (kushoto) na Gilbert Kigadye wakifuatilia kwa karibu mazoezi ya timu kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)

Shughuli ilikuwa kati ya Kelvin Nashot Naftal (kushoto) na Zuberi Rashid Ada.
Shughuli ilikuwa kati ya Kelvin Nashot Naftal (kushoto) na Zuberi Rashid Ada
Purukushani langoni ambako Dickson Job aliye hewani akikoa hatari langoni kwake.

MAJALIWA APOKEA MISAADA ZAIDI YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa Mstahiki Meya wa Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni tano kutoka kwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji ukiwa ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi 18,681,000/= kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea moja kati ya mabati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Eric Shigongo Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers (kushoto) ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisni kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 20 kutoka kwa watendaji wa kampuni ya Trans Ocean Supplies Limited ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 20 kutoka kwa mtendaji wa kampuni ya Woolworths Tanzania ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 50 kutoka kwa watendaji wa kampuni ya Pepsi ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
                                                                                            Msaada wa viti vya walemavu
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 415,800,000/= kutoka Chama cha Waagizaji wakubwa wa mafuta nchini (TAUMA ) ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea michango mbalimbali kwa ajili yawaathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, ofisini kwake jijini Dar es salaam
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea michango mbalimbali kwa ajili yawaathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, ofisini kwake jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata picha ya kumbukumbu na wachangiaji baada ya kupokea michango mbalimbali kwa ajili yawaathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, ofisini kwake jijini Dar es salaam
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 20 kutoka kwa watendaji wa kampuni ya Trans Ocean Supplies Limited ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akishukuru baada ya kupokea mchango wa shilingi 18,681,000/= kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 50 kutoka kwa watendaji wa kampuni ya Pepsi ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania, Roberto Jarrin (kushoto), Group Corporate Affairs Director wa TBL, Georgia Mutagahywa (wapili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa TBL, Fabian Mwakatuma baada ya kupokea hundi ya shilingi milioni 100 ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam

SERIKALI YARIDHIA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA-MAJALIWA

SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandariya Tanga nchini Tanzania.

Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo (tarehe 29 Septemba, 2016) Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.

Amesema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania.

Mradi huom kubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza Tanzania na Uganda.

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1,443 linatarajiwa kusafirisha mapipa 200,000 kwa siku ambapo kila pipa litaliingizia taifa Dola za Marekani 12.2.

Amebainisha kuwa pamoja na kusafirisha mafuta ya kutoka nchini Uganda bomba hilo pia linatarajiwa kusafirisha mafutakutoka nchi nyingine zaJ amhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudani Kusini ambazo zimeonesha nia ya kusafirisha mafuta yao kupitia bandari ya Tanga.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaja faida nyingine ambazo Tanzania itazipata kutoka na namradi huo kuwa ni kupatika na kwa ajira zaidi ya 15,000 wakati wa ujenzi na ajira 2,000 baadaya ujenzi kukamilika, kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia, kukuza biashara katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania, kampuni za ujenziza Tanzania kupata kazi za ujenzi.

Aidha, amesema Tanzania inatarajia kunufaika zaidi kwa kutumia bomba hilo kupitisha mafuta yanayotarajiwa kupatikana katika maeneo ya ziwa Tanganyika na Ziwa Eyasi.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM

JUMATANO, SEPTEMBA 28, 2016  

TRENI YAGONGA STESHENI NA KUUA MTU MMOJA NA KUJERUHI WENGI MAREKANI

Mtu mmoja ameripotiwa kufa na makumi kujeruhiwa, baadhi yao vibaya mno baada ya treni kugonga stesheni katika jimbo la New Jersey nchini Marekani.
Treni hiyo imeripotiwa kugonga kizuizi cha eneo la tiketi na kuingia katika eneo la mapokezi la stesheni ya Hoboken.
   Watu waliojeruhiwa wakiwa wamelazwa kwenye machela maalum za magari ya wagonjwa
             Mwanamke aliyejeruhiwa akiwa amewekewa kifaa maalum cha hewa ya oxygen
                    Waokoaji wakiangalia ndani ya treni kuangalia kama kuna watu waliojeruhiwa