Afisa masoko na mikopo wa benki ya Posta Tanzania tawi la Arusha Rafael Maganga akijitambulisha na kutoa maelezo kwa washiriki ni namna gani watanufaika na mikopo ya benki hiyo katika kukuza mitaji yao. |
Afisa Tawala wa jiji la Arusha Polycarp Laurent akiangalia Sabuni iliyotengenezwa na washiriki wa semina hiyo baada ya kufanya jaribio la kutengeneza sabuni ya maji kwa vitendo. |
Washriki wakiendelea na mafunzo yao kwenye ukumbi wa Kanisa la KKKT Kimandolu jijini Arusha |
Afisa mkuu wa kitengo cha Masoko na Mikopo wa Benki ya Posta Rafael Maganga akiwaeleza washriki wa semina ya ujasiriamali jinsi watakavyweza kupata mikopo kupitia Benki hiyo. |
Afisa masoko wa Benki ya Posta Tanzania Bruno Lanya akitoa Maelezo ya Kupata huduma za Benki hiyo kwa washriki wa semina hiyo picha zote na Mahmoud Ahmad wa globu ya jamii Arusha |
Na Mahmoud
Ahmad Arusha
Wajasiriamali
kote nchini wametakiwa kujitokeza kupata elimu ya ujasiriamali ilikuendana na
kauli ya mh.raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkta John Magufuli ya
Tanzania ya viwanda ambapo wametakiwa kujiongeza na kutafuta masoko ya bidhaa
sanjari na kutengeneza bidhaa zenye ubora.
Kauli hiyo
imetolewa kwenye Kata ya Muriet na katibu tawala wa wilaya ya Arusha mjini
Polycarp Laurent wakati wakitoa vyeti kwa washiriki wa semina ya wajasiriamali
zaidi ya 60 iliyoandaliwa na Taasisi ya Zebra Promotion yenye maskani yake jijini
Arusha.
Alisema kuwa
ili kuendana na kauli hiyo ifike mahali watanzania na wajasiriamali kujiongeza
kwa kutafuta na kutengeneza bidhaa zenye ubora utakaoendana na soko la hapa
nchini na nje ya nchi ambapo elimu ndio itakayowafanya kutoka eneo moja kwenda
jingine.
“Watendaji
na wenyeviti wa serikali ya mtaa wenye dhamana ya kuhakikisha ahadi ya mh raisi
inafanikiwa kwa kutoa ushirikiano kwa kampuni zenye nia ya dhati ya kutoa elimu
ya ujasiriamali kwa watanzania na yeyote atakayekaidi ahadi ya rais ataenda na
maji” alisema Laurent.
Akawataka
watendaji kushirikiana na taasisi mbali mbali zinazotoa elimu mbali mbali kwa
jamii na waache kufanyakazi kwa mazoea na kudai malipo ya kushiriki katika
kupatiwa elimu wa wananchi hilo ni kosa kisheria na linaweza kuwapeleka katika
vyombo vya sheria nawasihi muache mara moja tabia kama hizo.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Zebra Promotion Zuberi Mwinyi alisema kuwa jamii
ya watanzania itajitegemea iwapo kutakuwa na sera nzuri kama hili ya hapa kazi
tu nao watashirikiana na serikali katika kuhakikisha sera hiyo inafanikiwa kwa
vitendo na kuomba ushirikiano wa serikali.
Mwinyi
alisema kuwa mafunzo wanayotoa yana misingi ya kuwaunganisha wajasiriamali
katika vikundi ambavyo vinaweza kukopesheka kwa taasisi za kifedha na kuweza
kujiinua katika kutengeneza viwanda vidogo vidogo na baadae vya kati ambapo
mafunzo hayo yanalenga kuinua sera na kauli ya mh.Magufuli kwa kila kaya kutoa mjasiriamali mmoja.
“Mafunzo
yetu yanaenda sambamba na kauli mbiu yetu ya Tanzania ya viwanda inaewezekana,
ambapo mafunzo yetu yatatolewa katika mkoa wote wa Arusha zikiwemo wilaya za ArushaMjini,Monduli,Longido,Karatu,Arusha Dc,Meru na Ngorongoro na baadae Tanzania
kwa ujumla”alisema Mwinyi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni