Mgombea wa Republican Donald Trump
amelazimika kuondolewa haraka jukwaani na maafisa usalama katika
mkutano wake wa hadhara huko Reno, Nevada baada ya kutishiwa usalama
wake.
Katika tukio hilo mwanaume mmoja
aliyekuwa amebeba bango linalosema Republican wanampinga Trump,
alikamatwa na maafisa usalama baada ya kusema kuwa ana silaha, jambo
ambalo baadaye ilibainika kuwa si kweli.
Mgombea huyo wa Republican baadaye
alirejea jukwaani baada ya kuhakikishiwa usalama wake, na kusema kuwa
amejipanga kwenda kwenye majimbo ambayo ni ngome ya chama cha
Democratic.
Donald Trump akishikwa na afisa usalama na kuondolewa jukwani
Maafisa usalama wakimuondoa Trump jukwaani huku wakimkinga asiweze kudhuriwa
Mwanaume aliyedai kuwa na silaha akiwa chini ya ulinzi akisindikizwa na maafisa usalama
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni