Zaidi ya nyumbu 90 na swala 15 wamekufa katika eneo la mapito ya
wanyamapori, lililopo kwenye kata ya Selela wilayani Monduli mkoani
Arusha.nadaiwa kuwa wanyama hao wameangamia kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kimeta ulioibuka katika ushoroba huo wa Selela, unaoziunganisha mbuga za Tarangire na Hifadhi ya Ziwa Manyara, pia umeangamiza idadi kubwa ya wanyama wa kufugwa hasa ng'ombe, mbuzi na kondoo wapatao 60, huku idadi ya vifo ikitarajiwa kuongezeka.

Mkuu
wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta amesema baada ya matukio ya
wanyamapori kuanguka ghafla na kufa kwa wingi na baadaye mifugo pia
kuanza kuangamia, uongozi wa wilaya ulipeleka sampuli za mizoga hiyo kwa
Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi na ambaye alithibitisha
uwepo wa kimeta.
“Tunahofia
kuwa kimeta sasa kitakuwa kimesambaa maana wanyama kama nyumbu wana
tabia ya kuhamahama kutoka sehemu moja hadi nyingine, hivyo si ajabu
wamepeleka ugonjwa huu maeneo mengine," alisema.
Ofisa
Mifugo wilayani Monduli, Salum Omar amethibitisha kufa kwa ng'ombe,
mbuzi na kondoo kadhaa katika eneo lake na kuongeza kuwa hivi sasa
wameanza taratibu za kutoa chanjo dhidi ya maambukizi ya kimeta kwa
mifugo iliyobaki.
“Lakini
kuna haja pia ya kuhakikisha kuwa wafugaji, wengi wakiwa ni wa jamii
za Kimasai, wanapewa elimu juu ya mlipuko wa ugonjwa huu, maana wengi
wanakula mizoga ya mifugo yao iliyokufa,” alionya ofisa mifugo huyo.
Kwa kawaida binadamu akigusa mzoga wa mnyama aliyekufa kwa kimeta,
huweza kupata maambukizo hayo. Sasa wafugaji wa Monduli wanakwenda mbali zaidi, kula nyama iliyoathirika.
huweza kupata maambukizo hayo. Sasa wafugaji wa Monduli wanakwenda mbali zaidi, kula nyama iliyoathirika.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Selela, Julius Loiboseki ameomba msaada kwa serikali
iwasaidie kuzuia mifugo kutoka maeneo ya jirani ili isiingizwe kwenye
maeneo yao hadi pale tatizo litakapotatuliwa.
Kauli
hiyo imeungwa mkono na Diwani wa Kata hiyo ya Selela, Cuthbert Meela
ambaye alifafanua kuwa wilaya ya Monduli haijawahi mlipuko wa kimeta au
ugonjwa wowote ule mkubwa wa kutishia maisha ya
watu na wanyama.
watu na wanyama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni