Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiteta na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Tonia
Kandiero, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Mashauriano wa wadau wa
Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi),
Dkt. Leonard Chamuriho akitoa hotuba wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa 10
wa Mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga akitoa hotuba wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa 10
wa Mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Bi. Tonia
Kandiero, akitoa hotuba wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa 10 wa
Mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifungua
mkutano wa 10 wa Mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar
es Salaam.
Washiriki wa Mkutano wa 10 wa Mashauriano wa
wadau wa Sekta ya Uchukuzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi
wa mkutano huo, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwa katika
picha ya pamoja na wadau wa maendeleo alipofungua mkutano Mkutano wa 10
wa Mashauriano wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka
wadau wa Sekta binafsi kujitokeza na kushirikiana na Serikali katika
uwekezaji wa ujenzi wa miradi ya usafirishaji nchini.
Aidha
amewataka wadau hao kuendelea kufadhili utekelezaji wa miradi ya
maendeleo iliyo chini ya sekta hiyo ili kuchochea fursa za maendeleo.
Hayo
ameyasema wakati akifungua mkutano wa 10 wa mashauriano wa wadau wa
Sekta ya Uchukuzi na usafirishaji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
“Michango
ya Sekta binafsi inahitajika kwa kiasi kikubwa pamoja na Serikali
kuendelea kutenga fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo”, amesema
Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amesema kuwa mafanikio ya malengo ya mwaka jana ya mkutano huo
yamepelekea Serikali kupitia sekta hiyo kuboresha usafiri wa anga kwa
kununua ndege mbili za Bombadier Q400 mwaka huu.
Ameongeza
kuwa kwa sasa Serikali ipo katika hatua za awali za ununuzi wa ndege
nyingine tatu ambazo ndege ya kwanza itawasili Mwezi Julai mwakani na
nyingine mbili zitawasili mwezi Mei na Septemba 2018.
“Mapitio
ya mkutano wa 9 ni matunda ya upatikanaji wa ndege za Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL), hivyo mikutano kama hii ina tija kwani inaisaidia
kuboresha hali ya miundombinu nchini”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.
Amesisitiza
wadau kutumia mkutano huo kama chachu ya kupata maoni na mawazo mapya
ambayo yatasaidia katika kufanikisha uboreshaji wa Sera, Sheria na
kanuni za sekta ya usafarishaji nchini.“Tumieni
mkutano huu kujadili na kushauriana ili kupata majawabu yatakayosaidia
kutatua changamoto zilizopo katika Sekta hii”, amesema Prof. Mbarawa.
Naye,
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Tonia
Kandiero ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa maendeleo katika uboreshaji na ukuzaji wa Sekta ya
Usafirishaji ambayo ni kiungo kikubwa katika kukuza pato la Taifa.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Uchukuzi), Dr.
Leonard Chamuriho amesema kuwa anaimani mkutano huo utasaidia kutatua
changamoto za miradi mbalimbali iliyokuwa ikisuasua katika Sekta yake.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga amesema
kuwa sekta yake imefanikiwa kuunganisha kwa kiwango cha lami barabara
zote ndani ya mikoa na nchi jirani ambapo kwa sasa sehemu iliyobaki ni
kuunganisha ukanda wa Magharibi.
Amezitaja
barabara ambazo zipo katika ukanda huo kuwa ni Manyoni-Tabora-kigoma,
Kigoma-Kidahwe-Kasulu, Kibondo-Nyakanazi,
Sumbawanga-Mpanda-Uvinza-Kasulu, Tabora-Koga-Mpanda,
Mbeya-Chunya-Makongorosi-Rungwe na Itigi mpaka Mkiwa.Mkutano
huo wa siku moja umewashirikisha wadau wa Sekta ya Uchukuzi na
wafadhili mbalimbali katika kujadili miradi na utekelezaji wake pamoja
na kutafuta suluhu za changamoto zinazoikabili sekta.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni