Mwenyekiti
wa Ujumbe maalum wa wadau wa Ujenzi, Bi. Elizabeth Tagora (wa kwanza
kulia), akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini
(TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (wa kwanza kushoto), wakati ujumbe huo
ulipokagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la tatu la Abiria (Terminal
III) katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA).
Mkurugenzi
wa Mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), Eng. Mohamedi
Milanga akifafanua jambo kwa ujumbe maalum wa wadau wa ujenzi
walipokagua hatua za ujenzi wa jengo hilo.
Mkurugenzi
wa Mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), Eng. Mohamedi
Milanga akionesha wajumbe maalum wa wadau wa ujenzi eneo la kupumzikia
abiria katika Jengo la Tatu la Abiria (TB III) waliokagua hatua za
ujenzi wa jengo hilo.
Muendelezo
wa jengo la tatu la abiria sehemu ya pili katika hatua za ujenzi. Jengo
hilo litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 2,800 kwa
wakati mmoja.
Muonekano wa eneo zitakapokuwepo huduma za kibenki na Idara ya Uhamiaji katika Jengo la tatu la Abiria (TB III).
Muonekano
wa sehemu ya mbele ya wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III) katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA). Jengo hilo
linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka ujao.
Muonekano wa juu wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni