Na,Jumbe Ismailly,Igunga Nov,02,2016 Taarifa
BARAZA
la kawaida la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora
limeikataa taarifa ya utengenezaji wa madawati ya Halmashauri hiyo,kwa
masharti ya kumtaka aliyetoa taarifa ya kumdanganya Rais,Dk.John Pombe
Magufuli aende kwenye vyombo vya habari kukanusha taarifa hizo.
Mapema
julai,30,mwaka huu wakati wa ziara yake wilayani Igunga,Mkoani
Tabora,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli
julai,alikabidhiwa taarifa ya wilaya hiyo inayosema wilaya ya Igunga
haina upungufu wa madawati na kibaya zaidi kwa mujibu wa taarifa hiyo
ilikuwa na ziada ya madawati mia mbili.
Maamuzi
ya Madiwani hao yanafuatia taarifa ya utengenezaji wa madawati
iliyotolewa na afisa elimu wa wilaya hiyo, Mwisungi Kigosi kwenye
mkutano wa kawaida wa baraza hilo kuonyesha mabadiliko ya takwimu
zilizotolewa kwa Rais na walizosomewa madiwani hao.
Wakichangia
kwa nyakati tofauti hoja hiyo baadhi ya madiwani,diwani wa viti maalumu
CHADEMA,Anna Nyarobi,Charles Bomani wa kata ya Igunga,Gedi Nkuba wa
kata ya Nguvumoja na Henry Saidi wa kata ya Mwamala walisema kuwa
kuokana na taarifa hiyo kukinzana,kuwa na mkanganyiko na taarifa
iliyotolewa kwa Rais na kutokuwa vizuri,hawatakuwa tayari kuipokea
taarifa hiyo na kuirudisha kwenye kamati ya madawati wakaipitie tena
upya na kisha kuipeleka kwenye baraza maalumu la madiwani.
Anna
Nyarobi ni diwani wa viti maalumu kupitia CHADEMA akichangia hoja hiyo
alipendekeza kwamba watu waliotoa taarifa za uongo waende kwenye vyombo
vya habari na kukanusha taarifa hiyo kwa kusema kuwa taarifa waliyotoa
ilikuwa ni ya uongo,ili waweze kurudisha imani za wananchi kwa madiwani
wao.
Hata
hivyo diwani,Gedi Nkuba alibainisha kuwa kutokana na kuwepo kwa upungufu
wa madawati,alishauri Mkaguzi wa ndani afuatilie taarifa ya madawati
hayo pamoja na tathimini ya fedha zote zilizokusanywa kwa ajili ya
utengenezaji wa madawati hayo iweze kubainika.
Naye
diwani wa kata ya Mwamala,aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa Tume ya
kufuatilia utengenezaji wa madawati,Henry Saidi kwa upande wake
alibainisha kwamba,baada ya kubaini kuwepo kwa mianya ya ufujaji wa
fedha za madawati ya Halmashauri ya Igunga,walishindwa kuendelea na
mchakato huo wa utengenezaji wa madawati.
Afisa
elimu wa shule za msingi wilaya ya Igunga,Mwisungi Kigosi katika taarifa
yake aliyotoa kwa madiwani hao inaonyesha kwamba hadi kufikia
sept,21,mwaka huu wilaya hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 2,232 na
baada ya kukarabati madawati 725,upungufu halisi uliopo kwa sasa ni
madawati 1,507.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya
Igunga,Revocatus Kuul alisema alipotembelea katika shule ya msingi
Ganyawa alikuta wanafunzi wakiwa wanaendelea na masomo huku wakiwa
wamekaa chini.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Peter Onesmo aliwashauri madiwani hao
kutofanyika kwa baraza maalumu na lakini kutokana na mvutano wa maamuzzi
ya madiwani hao,ndipo walilazimika kupiga kura na baada ya kupiga kura,
madiwani wote walikubaliana kufanyika kwa baraza maalumu kwa ajili ya
kutatua tatizo la taarifa ya upungufu wa madawati hayo.
“Wanaosema
tuite baraza maalumu au tuunde kamati ndogo itakayoshirikiana na kamati
ya fedha,wanaosema tupeleke kwenye kamati ya fedha wainue
mikono,wanaosema kuwe na baraza maalumu wainue mikono,wanaosema liitwe
baraza maalumu wameshinda”alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Halmashauri
huku akishangiliwa na wajumbe wa mkutano huo.
Ni
Mweka hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Bwana Gordon Dinda.(wa
pili kutoka kulia) akisikiliza taarifa mbali mbali za kamati za kudumu
huku akilazimika kutolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoulizwa na
madiwani hao.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Ni
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani
Tabora,Bwana Revocatus Kuul(wa kwanza kutoka kulia) akiwa na Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo,Bwana Peter Onesmo wakati wa mkutanao wa kawaida wa
baraza la madiwani walipokuwa wakisomewa taarifa ya utengenezaji wa
madawati,taarifa ambayo waliikataa baada ya kubaini kuwa taarifa
iliyotolewa julai,30,mwaka huu kwa Rais,wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli ilikuwa ya uongo.
Ni
Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Bwana John Mwaipopo akifungua
mkutano wa kawaida wa barazaa la madiwani wa Halmashauri yaa wilaya ya
Igunga.
Ni
Afisa elimu shule za msingi,Bwana Mwisungi Kigosi akitoa taarifa ya
utengenezaji wa madawati kwa madiwani wa Halmashauri hiyo,ambayo hata
hivyo ilikataliwa baada ya kubainika haikuwa ikisema kweli.
Ni
Diwani wa viti maalumu (CHADEMA),Bi Anna Nyarobi(wa kwanza kutoka
kushoto) akisikiliza kwa makini taarifa ya utengenezaji wa madawati
iliyotolewa na afisa elimu wa shule za msimhi katika wilaya ya
Igunga,Bwana Mwisungi kigosi(hayupo pichani) ambayo hata hivyo madiwani
hwa kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vyao waliikataa na kuagiza
kiandaliwe kikao maalumu cha baraza hilo kwa ajili ya aliyetoa taarifa
za uongo kwa rais kwamba wilaya hiyo haina upungufu wa madawati wakati
bado yanahitajika zaidi ya madawati 1,500 akatangaze kwa waandishi wa
Habari kuwa alisema uongo kwa mkuu wa nchi..
baaddhi
ya madawati yaliyotengenezwa na Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani
Tabora kwa ajili ya kusambaza katika shule za msingi na sekondari
zilizopo kaatika wilaya hiyo..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni