Mwenyekiti wa Jukwaa la Habari Tanzania (TEF), Theothil Makunga (kulia),
akiwa na wajumbe wa jukwaa hilo, Jane Mihanji (katikati) baada ya
kutoka bungeni Dodoma jana, kusikiliza mwenendo wa majadiliano ya
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari.
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akiongoza majadiliano hayo
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani (kulia) akiwa na wapiga kura wake waliotembelea Bunge jana.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwasilisha bungeni Dodoma, Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipongezana na
naibu wake, Anastazia Wambura baada ya kuwasilisha muswada huo
Mbunge wa Tunduma, Mwakajoka akisalimiana na Mbunge wa Busanda, Leonecia Butimbaa
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati)
akijadiliana jambo na Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEA), Jane
Mihanji (kulia) na Saedy Kubenea kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma, baada
ya kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari.
Waziri
Kivuli wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi
akiwasilisha bungeni, Dodoma jana, maoni ya Kambi rasmi ya Upinzani
kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
Mbunge wa
Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akichangia hoja bungeni Dodoma,
kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, ambapo
alisema kuwa muswada huo hauwatendei haki wanahabari.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saedy Kubenea akichangia muswada huo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni