Balozi
Liberata Mulamula akiwasili nje ya jengo lenye studio ya Kilimanjaro
tayari kuongea LIVE katika kipindi cha Jukwaa langu kinachorushwa kila
siku ya Jumatatu kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku saa za Mashariki
za Marekanui. anayemfungulia mlango ni Abdul Malik
Balozi
Liberata Mulamula akiingia ndani ya studio akiwa amesindikizwa Harriet
Shangarai (kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa studio hiyo, kulia ni
Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme na Abdul Malik
Balozi
Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa studio meneja ambaye pia
ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Jukwaa langu, Bwn. Mubelwa
Bandio (hayupo pichani) Kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme
akifuatilia maelezo hayo.
Mhe.
Liberata Mulamula akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa meneja wa
studio Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi
cha jukwaa lako. Kati ni matangazaji maarufu wa Radio ya Times FM na
aliyewahi kutangaza Radio One Bi. Rose Chitalah ambaye pia anamsaidia
Mubelwa Bandio katika utangazaji na kuchangia hoja mbalimbali katika
kipindi cha Jukwaa langu.
Balozi
Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri
Mubelwa Bandio (kulia) na Rose Chitalah (hayupo pichani ) na
wasikilizaji waliokua na shahuku ya kumuuliza maswali.
Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji
mahiri Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani ) na Rose Chitalah (kushoto)
Kutoka
kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme, Mhe. Balozi Liberata Mulamula
na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakiwa katika picha ya pamoja.
Kutoka
kushoto ni Dj Luke Joe, Meneja wa studio ya Kilimanjaro, Mubelwa
Bandio, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah
wakipata picha ya kumbu kumbu na Balozi Liberata Mulamula anayemaliza
muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marejkani na Canada na sasa ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni