Mgeni
 rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof Mkenda  Akiwa na 
Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam life Insurance Ndg.Julius 
Magabe Tayari kwa Uzinduzi wa  Kampuni ya Sanlan.
 
Mtendaji
 Mkuu wa umoja wa makampuni ya Sanlam.Ndugu.Ian Kirk..Israel Kamuzora, 
Kamishna wa Bima katika Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Mara baada 
Uzinduzi wa wa Kampuni ya Sanlan wakionyesha Mshikamano.
Kampuni inayoongoza katika bima za maisha nchini, African life .
Assurance(Aflife) jana usiku wa Agosti 12, 2015 ilitangaza rasmi Kubadilisha jina lake la kibiashara na kuwa Sanlam Life Insurance ambayo ni Kampuni ya kimataifa ya huduma za kifedha yenye makao yake makuu Afrika ya Kusini, ambayo imekuwa na umiliki mkubwa zaidi wa hisa za kampuni hiyo tangu mwaka 2005.Badiliko hili ni kwa mujibu wa umoja wa makampuni ya Sanlam yenye lengo la kupanua wigo na kuimarisha uwepo wake nchini TanzanianaAfrika Mashariki kwa ujumla.Kwa upande wa wateja, wanahisa, mawakala na wafanyakazi, badiliko hili kuwa Sanlam Life Insurance litaimarisha faida za ushirika zilizojengwa kwa miaka 10 sasa.
Assurance(Aflife) jana usiku wa Agosti 12, 2015 ilitangaza rasmi Kubadilisha jina lake la kibiashara na kuwa Sanlam Life Insurance ambayo ni Kampuni ya kimataifa ya huduma za kifedha yenye makao yake makuu Afrika ya Kusini, ambayo imekuwa na umiliki mkubwa zaidi wa hisa za kampuni hiyo tangu mwaka 2005.Badiliko hili ni kwa mujibu wa umoja wa makampuni ya Sanlam yenye lengo la kupanua wigo na kuimarisha uwepo wake nchini TanzanianaAfrika Mashariki kwa ujumla.Kwa upande wa wateja, wanahisa, mawakala na wafanyakazi, badiliko hili kuwa Sanlam Life Insurance litaimarisha faida za ushirika zilizojengwa kwa miaka 10 sasa.
Kwa
 mujibu wa Bw Magabe, Sanlam Group ni kampuni ya kuheshimiwa Afrika 
yenye matawi  katika nchi 12. "Kwenye suala la wateja kuridhika na 
uaminifu, Sanlam imekuwa ikiipa sekta ya bima ya maisha kipaumbele kwa 
wakazi wa Afrika Kusini. Vile vile, kwa Tanzania Aflife daima imekuwa 
ikisifika kwa kuwa na huduma bora kwa wateja na kupewa alama za AA-na 
kampuni ya viwango ulimwenguni ya Global Credit Rating (GCR) kwa nguvu 
ya kifedha na ulipaji bora wa madai.”mabadiliko kutoka Aflife kuwa 
Sanlam Life Insurance yatachangia utendaji wa kibiashara kwa kampuni. 
"Kuna mipango ya kupanua soko la rejareja na kutoa huduma za ziada 
zilizo endelevu katika ukuzaji wa biashara, wateja wa Sanlam Life 
Insurance watapata bidhaa mpya zilizoboreshwa zaidi.”
Kupitia
 Sanlam, wateja wetu watakuwa na amani ya kufanya biashara na kampuni 
yenye masoko mengi Afrika inayoongoza katika kuimarisha ukwasi na 
usalama wa fedha. Tunatazamia kutumia fursa hii kuimarisha biashara yetu
 pamoja na uhusiano na wateja, washirika wetu, na zaidi mfumo wa Sanlam 
wa kufanya biashara kwa wingi na wateja. Tunapenda kuwahakikishia wateja
 wetu kuwa Sanlam ina historia ya miaka 97 ya utendaji  kazi na 
mahusiano bora na wateja wake. 
Bw.
 Kirk anaendelea kwa kusema, "Sanlam inajulikana kwa kauli mbiu ya 
“Wealthsmiths™” ambayo ni kielelezo tosha cha kile tunachokifanya na 
kuamini.Hiii na wakilisha itikadi ya uhalisia wa namna ya utendaji kazi,
 falsafa na uthamini wa rasilimali tunayoifanyia kazi ambayo ni fedha ya
 wateja wetu.Tunaelewa kiundani kuwa ukwasi unahitaji utendaji wa hali 
ya juu n akujitoa, kwa kutambua hili tunashirki kikamilifu na kwa 
umakini.” Huduma zetu zinauhalisia wa kile ambacho tunacho kithamini na 
pia tunafuata mfumo wa Sanlam ambao ni ujasiri, imani pamoja na ushujaa.
 Kwa kufuata mfumo na utamaduni huo, huduma zetu zimekuwa bora zaidi 
siku zote. 
Ikiwa
 na rekodi ya zaidimiaka 97, umoja wa makampuni ya Sanlam ina huduma 
tofauti za kifedha pamoja na mali zisizohamishika zenye thamani zaidi ya
 dola za Kimarekani bilioni 60na imesambaa sehemu mbalimbali duniani. 
SEM(Idara Ya Masoko yanayokuwa)inawajibika kwa huduma za kifedha za 
Sanlam kwa biashara katika masoko yanayokuwa nje ya Afrika Kusini, na 
inalenga kuhakikisha utoaji endelevu wa huduma na ukuaji katika biashara
 mbalimbali kwa kutumia nguzo hii
Mgeni
 rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof Mkenda  Akitoa Hotuba yake
 ambapo alipongeza Kampuni hiyo kwa Kuwa Mfano wa Kuigwa na Kuitaka 
Kuongeza Juhudi zaidi ili kupiha hatua.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni