Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Ole
Nangole kulia akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya
kuhamia rasmi chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Isaac Joseph Maarufu kama Kadogoo(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Chama cha Mapinduzi kimeendelea kupoteza wanachama wake mara baada Mwenyekiti
wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole pamoja na Katibu Mwenezi
wa Mkoa huo Isaac Joseph kutangaza rasmi kukihama chama hicho cha CCM na
kujiunga na CHADEMA.
Uamuzi
huo ulifanyika jana jijini Arusha katika moja ya hotel maarufu ambapo
viongozi hao walipata wasaa wa kupokelewa na uongozi wa chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Ole Nangole wakati
akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchama wa chadema
alisema kuwa CCM hivi sasa imekosa misingi iliyounda chama hicho ya haki
na usawa na kuongeza kuwa hivi sasa kimekuwa ni chama cha watu wachache
ambao wamekuwa wakichukuaa maamuzi kwa faida yao.
“Nasema
CCM imekosa misingi iliyounda chama hiki hakuna haki yeyote
inayotendeka imekuwa chama cha watu Fulani ambao wamekuwa wakichukua
maamuzi ya kukurupuka kwa faida yao”alisema Nangole
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Isaac Joseph Maarufu kama Kadogoo alisema kuwa
kudhirisha kuwa CCM sasa inaendeshwa kwa maslahi ya watu wachache,
mchakato wa kumpata mgombea Urais wa CCM uligubikwa na mizengwe na
kusema kuwa kama kanuni na taribu zingefuatwa ni Edward Lowasa ndiye
angechaguliwa katika mchakato ule.
Pia
alisema kuwa hawezi kukaa na kuongoza katika chama ambacho wafuasi wake
wamekihama ,huku akidai kuwa kwa Arusha mjini alikuwa na wafuasi elfu
ishirini na saba na waliojitokeza kupiga kura ya maoni ya kumpendekeza
mgombea ubunge kupitia CCM ni elfu tano
“ Siwezi kubaki kuongoza katika chama ambacho
kinabaka demokrasia Uongozi wa CCM watafute viongozi wengine wa
kuongoza chama hicho siko tayari na siwezi tena”alisema Kadogoo
Mwenyekit
wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Magoma Derick Magoma akiwapokea wanachama
hao kutoka CCM na kuhamia rasmi CHADEMA anawakaribisha wote wanaoijisika
kuunga nao na kuleta mabadiliko ya kweli kwa maslahi ya Taifa kwa
ujumla
“Tunawakaribisha
wote wanaotaka kuhamia chadema mlango upo wazi mda wowote na siku
yeyote mda wa mabadiliko ni sasa”alisema Magoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni