STARS YAJIFUA UTURUKI


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro ambayo iliwasili jana nchini Uturuki, imeendelea na mazoezi leo asubuhi katika viwanja viliyopo kwenye viunga vya hoteli ya Green Park – Kartepe.

Mara baada ya kuwasili jana jioni katika eneo la Kartepe, timu ilifanya mazoezi jioni kwa takribani saa moja na nusu, kuanzia saa 1 jioni mpaka mida ya saa 3 kasoro usiku, ambapo leo na kesho itafanya mazoezi asubuhi na jioni.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema huduma na vifaa vilivyopo katika hoteli waliyofikia (viwanja, gym) wanavyotumia kwa ajili ya mazoezi ni vizuri, hivyo ratiba yake ya mazoezi inakwenda kama alivyopanga katika maandalizi ya wiki moja ya kuajiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa mazoezi na timu ya Taifa ya Libya siku ya ijumaa, ambapo kocha Mkwasa atatumia nafasi hiyo kupima kikosi chake baada ya kuwa wamefanya mazoezi kwa siku nne nchini Uturuki.

Kikosi cha wachezaji 21 chini ya kocha mkuu Charles Mkwasa, na msaidizi wake Hemed Morocco, kocha wa makipa Peter Manyika na mshauri wa benchi la ufundi Abdallah Kibadeni wanaendelea kuwanoa vijana vilivyo kwa ajili ya mchezo wa mwezi Septemba dhidi ya Nigeria.Wachezaji waliopo kambini nchini Uturuki ni magolikipa Ally Mustafa, Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Abdi Banda, Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub.

Viungo ni Frank Domayo, Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said Ndemla na washambuliaji ni Saimon Msuva, Deus Kaseke, John Bocco, Rashid Mandawa na Farid Musa na Ibrahim Hajibu. 

Mlinda mlango Aishi Manula hakuweza kusafiri na timu kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii siku ya jumamosi kati ya timu yake Azam FC dhidi ya Yanga SCBathez kama anavyofahamika kwa washabiki na wapenzi wa mpira wa miguu ukanda wa Afrika Mashariki, amekua akiitumikia timu ya Taifa kwa vipindi mbali mbali tangu mwaka 2008.

Uwezo wake wa kuwapanga mabeki na kuongea nao wakati wa mchezo, kuokoa michomo ya hatari kutoka kwa washambuliaji, imeendelea kuwa sifa kubwa kwa mlinda mlango huyo ambaye pia amewahi kuzichezea timu za Simba SC na Ashanti United za jijini Dar es salaam.

Kipa huyo ni kipa wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013, 2014/2015 na washindi wa Ngao ya Jamii 2015/2016. Licha ya kutwaa ubingwa huo wa VPL akiwa na Yanga pia aliwahi kutwaa ubingwa huo akiwa na klabu ya Simba SC. Aidha kipa huyo pia ni mshindi wa kombe la Kagame mwaka 2012.

Barthez ana uzoefu mkubwa katika mashindano ya kimataifa, kwani ameshafanikiwa kucheza michezo mingi yenye upinzani wa hali ya juu katika ngazi ya klabu na timu ya Taifa.

Kuelekea mchezo dhidi ya Nigeria, mlinda mlango huyo yupo vizuri na endapo mwalimu atampa nafasi atafanya vizuri katika kuperusha bendera ya Taifa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni