MKUU WA MKOA WA ARUSHA,FELIX NTIBENDA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE NJIRO

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Kanda ya Kaskazini(Taso)Arthur Kitonga akisoma taarifa ya Taso inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro,Manyara na Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara ambao ni wanachama wa Taso Kanda ya Kaskazini,Mh Joel Bendera akisistiza jambo kwenye mkutano wa ufunguzi uliofanyika kwenye viwanja ya Nanaenane Njiro jijini Arusha,anayesikiliza kwa makini ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda(wa pili kushoto).

Meneja wa Shama la Mbegu la Serikali mkoa wa Arusha,Zawadiel Mrinji akionesha mfuko ulitengenezwa maalumu kwa lengo la kudhibiti wadudu waharibifu baada ya mavuno ili kumwezesha mkulima kunufaika na mazao yake.

Meneja wa Shama la Mbegu la Serikali(ASA) mkoa wa Arusha,Zawadiel Mrinji akizungumzia umuhimu wa zao la Ngano linalostawi kwa wingi wilaya ya Monduli na Hanang .


Viongozi wa serikali wakikagua bustani ya JKT ambayo imekua kivutio kwa wananchi wanaotembelea maonesho ya Nanenane Njiro mkoani Arusha.

Bustani  ya taasisi ya Utafiti wa Kahawa(Tacri)hutembelewa na wakulima kujifunza namna bora ya kilimo cha Buni nchini.


Wananchi wakipata maelezo kutoka kwenye banda la Sementi la Simba Cement .

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki Kuu(Arusha) ambao wanashiriki kwenye maonesho  hayo wakijumuika na wananchi kusikiliza hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Felix Ntibenda. 

Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)Oljoro mkoa wa Arusha wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi.

Wanafunzi wakiwa kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kujifunza mambo mbalimbali yanatolewa na Chuo hicho.

Kikundi cha burudani kutoka JKT Oljoro wakionesha ufundi wao wa ngoma kutoka Pemba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni