BAADHI ya
 wanahabari wa mitandao ya jamii jijini Dar es Salaam wamepewa mafunzo 
juu ya taarifa za uzazi na afya ya mama na mtoto ili waweze kuelimisha 
zaidi jamii kupitia mitandao yao dhidi ya taarifa hizo. Akizungumza 
wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza 
Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke 
Mwakatundu alisema taasisi yake imeamua kutoa mafunzo hayo kwa 
wanahabari hao ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii 
kupitia mitandao yao juu ya umuhimu wa kupambana na vifo vya mama na 
mtoto vinavyoendelea kutokea kila uchao. Alisema kazi ya kupunguza vifo 
vya mama na mtoto si jukumu la madaktari au hospitali pekee lakini 
jukumu la jamii nzima kukabiliana na huduma hiyo, alisema vyombo vya 
habari ikiwemo mitandao ya jamii inakilasababu za kuonesha mapungufu na 
kueleza changamoto katika huduma za afya zinazotolewa kwa lengo la 
kuboresha zaidi huduma hizo. Alisema tatizo la elimu ya afya ya uzazi ni
 kubwa nchini kwani takwimu zinaonesha kwa kila saa moja kuna mama 
anayepoteza maisha kutokana na matatizo ya uzaziSerikali. "...Kila siku 
kuna akinamama takribani 24 wanapoteza maisha kutokana na matatizo ya 
uzazi nchini," alisema Dk. Mwakatundu. Awali akizungumzia hali halisi ya
 uzazi wa mpango nchi, Meneja Mawasiliano wa WLF, Victoria Marijani 
alisema kuna faida kuwa ya kuzingatia Uzazi wa Mpango kwani ni uwekezaji
 wenye faida na endelevu ambao unachangia kupunguza vifo vitokanavyo na 
uzazi kwa kiasi kikubwa hadi asilimia 44. Aliongeza kuwa uwekezaji huo 
wa ziada katika afya, elimu, usawa wa kijinsia na uwepo wa sera wezeshi 
za kiuchumi vitaiwezesha nchi kupata manufaa yatokanayo na ukuaji wa 
haraka wa uchumi. Alisema familia zinazotumia uzazi wa mpango zinakuwa 
na uwezo wa kuwatimizia watoto mahitaji yao muhimu kama chakula, elimu, 
mavazi, huduma za afya na makazi. "...Atapata muda wa kushiriki katika 
shughuli za jamii, Atamudu kujiwekea akiba, Atakuwa na amani na upendo 
kwa familia yake. Alisema kiwango kikubwa cha vifo vya watoto chini ya 
miaka 5 (vifo 81 kwa vizazi hai 1000) Kiwango kidogo cha utumiaji wa 
njia za kisasa za uzazi wa mpango (Asilimia 27). Wastani wa utumiaji wa 
njia za kisasa za uzazi wa mpango hapa nchini bado ni mdogo. Ni asilimia
 27 tu ya wanawake walio kwenye umri wa kuzaa ndio wanaotumia njia za 
kisasa za Uzazi wa Mpango.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni