Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva
(katikati) akizungumza na waandishi habari juu juu ya maendeleo
mbalimbali katika kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu ya
NEC jijini Dar es Salaam,Kulia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam,Kamishina Suleiman Kova na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji
Uchaguzi,Clothilde Komba.
Kamanda
wa polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova
akizungumza na waandishi habari juu juu jeshi la polisi lilivyojipanga
katika suala la ulinzi kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao
Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam.
Waandishi
wa habari wakifatilia wa taarifa ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es
Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TUME ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuanza kutoa fomu ya urais ,Ubunge
pamoja na Udiwani kesho na kumalizika kwa zoezi la utoaji fomu hizo ni
Agasti 21 mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu,Damian Lubuva amesema wakati wa
uchukuaji wa fomu ya urais itatolewa bure lakini wakati wa kurudisha
anatakiwa kuweka dhamana ya Sh.milioni Moja na wadhamini wadhamini 200
katika kila mkoa na kuwepo kwa mikoa miwili Zanzibar.
Lubuva
a amesema kuwa wakati wa kuchukua fomu viongozi wa vyama vya kisiasa
wanatakiwa kuchukua fomu na kurudisha bila kuwa na kundi kubwa ambalo
linaweza kusimamisha shughuli za watu wengine.
Amesema
kwa fomu za ubunge ni sh.50,000 na udiwani sh.5000 ambapo wanatakiwa
kuchukulia katika ofisi za wilaya na uchukuaji huo lazima uwe wa
kistaarabu katika kuweza watu wengine waendelee na shughuli zao.
Lubuva amesema kuwa wanasiasa wanatakiwa na lugha za kistaarabu katika mikutano yao katika kujenga demokrasia iliyo ya ukweli.
Hata
hivyo amesema kuna baadhi ya vijana wanauza kadi za tume ya taifa ya
uchaguzi na kutaka vyombo vya usalama kuchunguza pamoja na kuwachukulia
hatua watu wanaouza kadi hizo.
Kamanda
wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova
amesema kuwa uchaguzi unaendana na usalama hivyo jeshi limejipanga
katika ulinzi katika kipindi hiki.
Kova amesema kuwa Jeshi litaendelea kushirikiana na viongozi wa siasa katika kuleta amani katika kipindi cha uchaguzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni