fomu  ya  mgombea  wa  Chadema ubunge  Ludewa zikiwa  hazijatimia baada ya tomu ya  tamko kukosekana
Fomu ya  mgombea  wa Chadema  ikiwa haijazwa senemu ya  tarehe ,mwezi na mwaka
Mzee  Kada  wa Chadema  akimpongeza  mbunge wa  Ludewa  Deo Filikunjombe  baada ya  kupewa  barua ya kupita  bila  kupingwa
Mbunge  wa  Ludewa  Deo  Filikunjombe  akizungumza na  wanachama  wa CCM na  wananchi wa Ludewa baada ya  kupita  bila  kupingwa
Filikunjombe  akionyesha  barua ya  kupita  bila  kupingwa
Msimamizi
  wa uchaguzi jimbo la  Ludewa Bw Wiliam Waziri akimpongeza  mbunge  
Filikunjombe  baada ya  kumkabidhi barua ya  kupita  bila  kuingwa  
ubunge jana 
Na Matukiodaima Blog
ALIYEKUWA
  mbunge   wa  jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe (CCM)  amepita  bila 
 kupingwa  baada ya  mgombea  wa chama  cha Demokrasia na maendeleo 
(chadema) Barthomew Mkinga  kushindwa kutimiza Masharti na Taratibu za 
Ujazaji wa Fomu.
Msimamizi
 wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa Bw  Wiliam Waziri alisema  jana   kuwa 
Mgombea wa Chadema ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo 
hivyo kukosa sifa ya kuwa Mgombea wa Ubunge hivyo  kumkabidhi  barua  
rasmi Filikunjombe   ya kupita  bila  kupingwa
Waziri alisema   kwamba Kati ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni Mgombea wa CCM, Bw. Filikunjombe pekee;
Kuwa 
Wagombea wa DP na TLP walishindwa  kabisa kurejesha fomu huku Mgombea wa
 Chadema akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha Fomu ya 
Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi.
Mgombea  
 huyo  wa Chadema  aliyereja  fomu  ya  wadhamini  bila  kujaza tarehe  
,mwezi  wala mwaka ambao uchaguzi  mkuu utafanyika .
Kwa  
upande  wake  mgombea  ubunge  wa TLP Bw  Blanka  Haule  alisema  kuwa 
alishindwa kurejesha  fomu hizo  kwa wakati kutokana kukosa picha za  
kubandika katika  fomu hiyo  kutokana na  hali ya mazingira ya  Ludewa  
kukowa  eneo la  kupiga  picha hizo.
Kwani  
alisema picha  ambazo alipiga  Njombe  alizisahau  alikoziweka   hivyo  
kulazimika  kwenda kupiga  pich nyingine  za  haraka kwa  muda  wa 
dakika tatu  ila  cha  kushangaza dakika  tatu  za kutoka  picha  hizo  
zilionekana  kushindwa  kutoka kwa  wakati na kutoka  saa 11  jioni .
“Nilijipanga
  kugombea  ubunge  ili  kumpokea  ubunge  Deo Filikunjombe na  
kuendeleza  yale  yote aliyoyafanya  jimboni  ila watu  wa  picha  
walinikwamisha na  kushindwa kupata  picha kwa  wakati hivyo kwa  sasa  
ndio  basi  tena japo ilikuwa ni  Demokrasia lakini kapita  bila  
kupingwa  ndio mbunge wetu:”
Akizungumzia
  hatua ya  mgombea  wao wa Chadema  kushindwa  kukamilisha  taratibu  
za  ujazaji wa fomu  hizo Bw Daniel Songo alisema kuwa mgombea  wao 
hakuwa makini hata  kidogo kwani alikuwa ni mtu ambae hakutulia na muda 
 mwingi alikuwa akifikiria  juu ya  wanachama  wanaohama  chama na 
kuacha kutulia katika kujaza  fomu  hizo .
Japo  
alisema chama hicho  kimepoteza  umaarufu  kutokana na  mwenendo wa  
viongozi wa juu wa chama  hicho  kuendekeza  siasa za ukanda zaidi  na 
kuacha  kutazama uhai wa  chama   hicho.
Mwenyekiti
  wa CCM wilaya ya  Ludewa Stanle Kolimba  alisema  kuwa amepokea kwa  
furaha kubwa hatua ya  mgombea  wake wa nafasi ya  ubunge  kupita  bila 
 kupingwa na kuwa kazi kubwa kwa  sasa kuhakikisha mgombea  urais wa CCM
 Dr John Magufuli anapata  kura  za  kimbunga  pamoja na kupigania  kata
  zote kuona CCM .
Kwa 
upande  wake  Bw  Filikunjombe  akizungumzia hatua hiyo ya  kupita  bila
  kupingwa alisema ameipokea  kwa vizuri sana kwa  alitegemea wapinzani 
 hao  wajitokeze  ili aweze  kuwaonyesha kazi kwa  kuhakikisha  
wanaangukia  pua katika uchaguzi huo .
Alisema 
kazi  kubwa ya  maendeleo ambayo ameifanya katika  jimbo  hilo kwa miaka
  mitano na imani kubwa ambayo wananchi wa Ludewa wanayo dhidi yake 
ilikuwa ni  vigumu kwa  wapinzania hao kupata  kura Ludewa.
Bw  
Filikunjombe  aliwaomba  wananchi wa Ludewa kura  zote  ambazo  
walipanga  kumpigia  yeye kuzielekeza  kwa mgombea  Urais Dr Magufuli na
 kwa madiwani wa CCM na  furaha  yake  kuona wapinzani  wanaambulia  
patupu katika  wilaya ya  Ludewa






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni