Filamu
iliyopewa jina la AISHA imezunduliwa rasmi siku ijumaa ya tarehe
31/7/2015 wilayani Pangani chini ya shirika lisilo la kiserikali la
UZIKWASA.
Aisha
ni filamu ya tatu katika mfululizo wa filamu za UZIKWASA zikiangazia
aina mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa
kike. Filamu hizi ni ni sehemu mojawapo tu ya njia za mawasiliano katika
kampeni shirikishi-jamii ya mabadiliko ya tabia inayofahamika kama
'BANJA BASI'!, Pangani, Tanga.
Kabla
ya filamu ya Aisha iliyozinduliwa kwa kishindo hivi karibuni, shirika
la UZIKWASA tayari limeshatengeneza filamu nyenigne mbili ambazo ni
FIMBO YA BABA na CHUKUA PIPI, wengi wa waigizaji waliomo ni wasanii wa
vijijini.
Pia
filamu hizi zinatokana na maisha halisi na utafiti wa kina katika
jamii. Kwa nji hii UZIKWASA inahakikisha filamu zake zinaeleweka na
zinafanya kazi kama kioo wka jamii. Lengo ni tuone, tuguswe na hatimaye
tuchukue hatua ili kuleta mabadiliko.
Filamu
ya AISHA inamhusu mwanamke anayeishi mjini na kuamua kurudi kijijini
kwao kuhudhuria harusi ya mdogo wake. Wakati anajikumbusha maisha yake
ya zamani, na kukutana na familia yake pamoja na marafiki, kunatokea
mkasa wenye athari kubwa katika maisha yake.
Watu wangefumbia macho mkasa huo, lakini Aisha anaamua kupambana nao vikali ili kupata haki yake.
Filamu
hii inahusu unyanyaa, aibu na wahanga kulaumiwa, na namna gani inazuia
wanawake na wasichana kusema wazi. Pia inahusu baadhi ya mamlaka na
viongozi kusita kufatilia ukiukaji wa haki za binadamu.
AISHA
imeongozwa na mtaalamu maarufu Chande Omar, imetayarishwa kwa
ushirikiano na Kijiweni Production, imefadhiliwa na A. Schindler na
Swiss Development Cooperation (SDC) na kusimamiwa na shirika la
UZIKWASA.
Filamu ya aisha ni kwa heshima ya wanawake wote waliopitia mikasa ya namna hii.
Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Regina Chonjo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, nae alipata nafasi ya kutoa hotuba yake.
Producer wa filamu ya Aisha Bwana Emil Shivji akizungumza na wananchi waliohudhuria viwanja vya Bomani.
Mkurugenzi
wa shirika la UZIKWASA Dokta Vera Piroth akitoa hotuba yake ya kipeke
ambayo ilikuwa katika mtindo wa hadithi pamoja na maswali, Ilipendeza
sana.
Shamra
shamra za ngongoti zikikaribisha wageni waalikwa kwenye uwanja wa
Bomani wilayani Pangani palipofanyika uzinduzi wa flamu ya Aisha.
Msanii maafuru wa mashairi Ndugu Mabwingo akitoa burudani jukwaani.
Wananchi wakiendelea kufatilia uzinduzi wa filamu ya Aisha.
Msanii mahiri katika uimbaji, Vitalis Maembe alikuwepo kwenye uzinduzi wa filamu ya Aisha, alitoa burudani ya kipekee.
Wasanii waliocheza filamu ya Aisha wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakipokea zawadi zao za ushiriki.
Washereheshaji
katika uzinduzi wa filamu ya Aisha, Mohammed Hammie maarufu kama Anko
Mo (kati kati), Nickson Lutenda aliyevaa koti la bluu pamoja na Pili
Mlindwa.
Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Regina Chonjo.
Msanii
Godliver Gordian ambaye amecheza kama Aisha katika filamu hiyo,
akifanya mahojino na kituo cha luninga cha TBC ambao walikuwepo katika
uzinduzi huo.
Msanii
Vitalis Maembe akiwa na Godliver Gordian (Aisha), wakati wa utambulisha
wa wimbo uliotumika kama soundtrack katika filamu hiyo.
Godliver
Gordian ama Aisha akiwa na mshumaa mara baada ya wananchi kuitazama
filamu ya AISHA- lengo la mshumaa huo ni kumulika unyanyapaa, pamoja na
aibu wanayoipata wanawake na wasichana wanapotendewa matendo maovu.
Wageni
waalikuwa wakiongoza na mkuu wa wilaya Pangani Bi Regina Chonjo nao
waliwasha mishumaa katika kumuunga mkono Aisha katika harakati za
kufichua maovu.
Wananchi wengine pia waliwasha mishumaa kuashiria kuunga mkono harakati hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni