Ninapenda
 kuwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama changu, CHADEMA, kwa 
kunipitisha kwa kura zote kuwa mgombea wa Urais kupitia muungano wa 
vyama vyetu, UKAWA. Kiupekee kabisa napenda kumpa shukrani na pongezi 
mgombea mwenza, Juma Duni Haji Kwa kukubali majukumu haya makubwa ya 
kuelekea
mabadiliko
 makubwa pamoja na Mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe kwa kusimama imara 
katika kipindi hiki kigumu. Nimewaambia wajumbe wa mkutano mkuu kuwa 
natambua kazi wanayofanya ni kubwa na wanajitolea, na kwa umoja wetu, 
tutafika kila jimbo na kufanya kampeni za kisayansi bila matusi na 
tutapata Ushindi wa Asubuhi Mapema. Asanteni sana kwa imani yenu kwangu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni