Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanga nyaraka vizuri kwenye meza kuu, kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kuanza leo, katika Ukumbi uliopo jengo la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma.
Baada ya kikao hicho kuanza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alitoka ukumbini na kuwaambia Waandishi wa Habari kwamba, moja ya maazimio ya Kikao hicho ni kwamba kura za maoni zitarudiwa keshokutwa Alhamisi, katika majimbo matano ya Ukonga, Kilolo, Busega, Rufiji na Makete ambako yamejitokeza malalamiko na kufika katika vikao vya Chama, kuhusiana na kura za maoni za awali
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili katika ukumbi uliopo jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuzungua kikao hicho. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula
Kikao cha Kamati Kuu kikiendelea
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Adam Kimbisa akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano CCM, Daniel Chongolo, baada ya kuwasili kwenye jengo la White House kwa ajili ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo
Mjumbe wa Kamati Kuu, Adam Kimbisa akiwasalimia wajumbe wenzake ukumbini kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. Kutoka kulia ni Shamsi Vuai Nahodha, Zakia Meghji na Dk. Salim Ahmed Salim
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Huseein Mwinyi, Samia Sluhu Hassan ambaye pia ni Mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM na Ameir Pandu Kificho wakiwa ukumbini kabla ya kikao hicho kuanza
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akijadili jambo na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib ukumbini. kushoto ni Katibu wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dr. Asha-Rose Migiro
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Zakiah Meghji na Dk. Asha-Rose Migiro wakibadilishana mawazo ukumbini
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi akimsalimia mjumbe mwenzake Dk. Hussein Mwinyi ukumbini.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa ukumbini kabla ya kikao kuanza
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa na Mzee Steven Wassira wakibadilishana mawazo ukumbini
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa na Dk. Emmanuel Nchimbi wakibadilishana mawazo ukumbini
Katibu wa Sekretarieti ya CCM, Anamringi Macha, akiratibu mambo kabla ya kikao hicho kuanza
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Maua Daftari na Mgombea Mwenza wa CCM, Samia Suluhu wakijadiliana mambo ukumbini
Wajumbe wa Kamati Kuu, Katibu w NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Megji walishauriana jambo kabla ya kikao hicho kuanza
Maofisa wa CCM wakiwa katika shughuli mbalimbali ofisini leo wakati kikao cha Kamati Kuu ya CCM kikiendelea. Picha zote na Bashir Nkoromo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni