Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa taasisi ya Young
Scientists Tanzania (YST), Dk. Gosbert Kamugisha, akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) leo hii wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya siku
tatu ya miradi na ubunifu wa kisayansi uliofanywa na wanafunzi kutoka shule
120 nchini. Maonyesho hayo yatafikia kilele Ijumaa Agosti 7, 2015. (Picha
zote na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).
Mwanzilishi Mwenza wa YST, Joseph Clowry, akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
hii.
Makamu wa
Rais wa kampuni ya kuchakata mafuta na gesi ya BG Tanzania, John Ulanga,
akizungumzia udhamini wao katika maonyesho hayo ya YST. Kampuni hiyo imetoa
kiasi cha Dola 200,000 kudhamini maonyesho ya mwaka
huu.
Naibu
Balozi wa Ireland nchini, Brian Noran, akizungumzia maendeleo ya tafiti za
kisayansi kwa taifa lolote duniani. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji na
Mwanzilishi Mwenza wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha.
Mkutano
ukiwaunaendelea.
Wanahabari wakiwa kazini.
Wanahabari wakifuatilia kwa makini.
Mwalimu
Geofrey Ndunguru (kulia) na mwanafunzi Yussuph Mwenda kutoka Shule ya
Sekonari ya Wavulana Songea nao wanashiriki maonyesho hayo kuzungumzia
Uchambuzi wa Mtazamo wa Wanafunzi Wasioona kuhusiana na
Sayansi.
Mwanafunzi Gladness Mpelemba (kulia) wa kidato cha tatu kutoka
Shule ya Sekondari Sumaye mjini Morogoro akielezea kuhusu utafiti wao wa
'Kutumia Njia za Asili za Kupanga Uzazi Kupunguza Madhara kwa Wanawake'.
Kushoto ni mwenzake Glory Crispine.
Wanafunzi
wakiendelea kuonyesha tafiti zao.
Mojawapo
ya utafiti uliofanywa na wanafunzi Saada Abeid na Zaina Maliki wa Shule ya
Sekondari ya Wasichana Mtwara.
Majaji
wakiwa kazini leo hii ili kuwapata washindi watakaotunukiwa zawadi
mbalimbali hapo kesho ambapo Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Alhaj Ali
Hassan Mwinyi, ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Na Daniel
Mbega
MAONYESHO
ya Tano ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini yamfunguliwa
rasmi jijini Dar es Salaam leo yakiwa yanaendeshwa na kuratibiwa na taasisi
ya
Young Scientists Tanzania (YST).Maonyesho hayo
ambayo yanafanyika kwenye Ukumbi wa iamond Jubilee yanashirikisha jumla ya
wanafunzi 240na walimu 120 kutoka shule 120 nchini yanatarajiwa kufikia
kilele
keshokutwa Ijumaa ingawa kesho Alhamisi zawadi mbalimbali zitatolewa kwa
washindi zikiwemo fedha taslimu, medali, vikombe, vifaa vya maabara pamoja
na
maktaba.
Dk.
Gosbert Kamugisha, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa
YST,
amesema mgeni rasmi atakayetoa zawadi kwa washindi hapo kesho atakuwa Rais
mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
“Maonyesho
haya ni kwa ajili ya kuonyesha ubunifu na utafiti wa kisayansi uliofanywa na
wanafunzi wa sekondari na katika kipindi cha siku tatu kuanzia leo wanafunzi
hao wataonyesha miradi mbalimbali katika maeneo tofauti ya kisayansi kama
kemikali, fizikia na sayansi ya hisabati, sayansi ya kibaolojia na
kiikolojia,
sayansi ya kijamii na kitabia, na teknolojia,” alisema Dk.
Kamugisha.
Aliongeza
kwamba,
kama njia ya kutambua kazi iliyofanywa na wanafunzi hao, ndiyo maana
wameandaa
zawadi mbalimbali kuwamotisha ambapo mbali ya zawadi zilizotajwa, pia
wanafunzi
sita wanaweza kupata udhamini (scholarship) kwa ajili ya masomo ya chuo
kikuu
kwa fani mbalimbali za sayansi na teknolojia, udhamini ambao hutolewa na
taasisi binafsi ya Karimjee Jivanjee Foundation ya jijini Dar es
Salaam.
“Maonyesho
ya mwaka 2015 ya YST yanalenga kuonyesha vipaji na ubunifu wa wanafunzi wa
sekondari, lakini pia ushuhuda wa umahiri wa mbinu za ufundishaji kwa walimu
ambao ndio wanaowaongoza wanafunzi hao yakiwa ni matunda ya mafunzo
yanayotolewa
na YST kwa walimu wa sayansi katika kipindi cha miaka minne iliyopita,”
aliongeza Dk. Kamugisha.
Amewataja
wadhamini
wakubwa wa maonyesho ya mwaka huu kuwa ni kampuni ya BG Tanzania
inayojihusisha
na masuala ya utafiti wa mafuta na gesi asilia pamojana Shirika la
Kimataifa la
Misaada la Ireland (Irish Aid).
Akizungumzia
mafanikio ya maonyesho hayo, Dk. Kamugisha alisema mwitikio umekuwa mkubwa
zaidi tofauti na walipoanza maonyesho hayo mwaka
2011.
“Wakati
tulipoanza mwaka 2011 walishiriki wanafunzi nane tu, mwaka 2012 wakawa 300
kwani zilikuwepo shule 100, mwaka 2013 walishiriki wanafunzi 200, mwaka 2014
pia walikuwepo wanafunzi 200 lakini mwaka huu wamekuwa 240 kwani hata shule
zimeongezeka kutoka 100 hadi 120.
“Tulipokea
maombi ya shule 400 nchi nzima, lakini tukaamua kuzichagua hizi 120.
Tulizitembelea
shule zote 400 mara tatu kwa mwaka, ndipo hatimaye tukaziteua hizi
zinazoshiriki ingawa tunaamini kwamba shule nyingi sasa zimehamasika na
watoto wanapenda
sayansi,” alisema.
Akizungumza
katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mwanzilishi Mwenza wa YST Joseph
Clowry, alisema kwamba kuna dalili za mafanikio tangu walipopata wazo la
kuanzisha taasisi hiyo mwaka 2009, kwani mwitikio umeonekana kuwa mkubwa
kadiri
miaka inavyokwenda.
Alisema,
ili taifa lolote liendelee, ni vyema kuwekeza zaidi katika tafiti za
kisayansi
kwa kuanzia kwenye ngazi za chini kabisa kama wao
wananvyofanya.
“Ireland
ilikuwa nyuma kimaendeleo kama zilivyokuwa nchi nyingi ulimwenguni, lakini
walipoamua kuwekeza kwenye sayansi hali imebailika hivi sasa ambapo wapo
wanasayansi mahiri kabisa na vijana nao wanapenda kujifunza masomo ya
sayansi,”
alisema Clowry.
Kwa upande
wake, Makamu Rais wa BG Tanzania anayeshughulikia Sera na Masuala ya
Uhusiano,
John Ulanga, alisema wameamua kujitolea kudhamini YST kwa sababu wanatambua
kwamba Tanzania inahitaji kuwa na wanasayansi wengi hasa tunapozungumzia
suala
la mafuta na gesi ambayo yakitafitiwa yakapatikana na kuchakatwa yanaweza
kuinua uchumi wa taifa kwa kiwango kikubwa.
“Tunahitaji
wanasayansi wa kutosha katika sekta hii adhimu ya mafuta na gesi, tukiwa nao
wazalendo itakuwa ni bora zaidi, hivyo ni lazima tuwadhamini watu kama YST
ambao wanajenga msingi imara katika kuwapata wataalamu wa kesho,” alisema
Ulanga.
Ulanga alisema
kwamba, kwa mwaka huu kampuni yake imetoa Dola 200,000 (takriban Shs. 450
milioni) kwa ajili ya udhamini wa maonyesho hayo na akaahidi kwamba
wataendelea
kudhamini kwa kadiri ya mahitaji na hali
itakavyoruhusu.
Naye Brian
Noran, Naibu Balozi wa Ireland nchini, amesema ni jambo la busara kwa
serikali
na jamii kuwekeza katika utafiti wa kisayansi kama kweli taifa linataka
maendeleo, lakini akaahidi kwamba serikali yake itaendelea kusaidia kwani
inatambua umuhimu wa kuwa na wanasayansi wabunifu.
Aliwapongeza
YST kwa hatua waliyoifikia mwaka huu na kuwahamasisha waongeze bidii zaidi
ili
kujenga taifa la wanasayansi kwa kuanzia ngazi ya
chini.
“Sayansi
ndiyo inayoweza kuleta mabadiliko na maendeleo, hivyo ni muhimu kuendelea
kuwazalisha wanasayansi ambao watakuja kuwa wabunifu wazuri hasa katika
karne
hii ya sayansi na teknolojia,” alisema Noran.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni