Mkuu
wa Masista Waabuduo Damu ya Kristo, Euprasia Julius akimtambulisha
mgeni rasmi na meza kuu kwa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe
(hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa
Maria De Mathias (MDM) Vikawe, Kibaha.
Na Mwandishi wetu, Kibaha
MGANGA
Mkuu wa halmashauri ya Mji Kibaha, Dk. Happniness Ndosi amepongeza
shirika la masisita wa Waabuduo Damu ya Kristo kwa kufanikisha ujenzi wa
zahanati ya kisasa katika kijiji cha Vikawe wilayani Kibaha mkoani
Pwani.
Mganga
huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa zahanati
hiyo,pamoja na kuwapongeza amesema serikali itaendelea kushirikiana na
mashirika yote kwa lengo la kuwezesha kila kijiji kiwe na zahanati na
kila kata kituo na kila wilaya kuwa na hospitali.
Aliwapongeza
masista hao kwa kuonesha upendo na huruma kama Biblia inavyomsimulia
msamaria mwema ambaye alikuta mtu aliyepigwa na majambazi na kumsaidia.
Mganga
Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akimpa
mkono wa shukrani Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa
Italia, Germano Frioni kwa ujenzi wa Zahanati hiyo itakayohudumia wakazi
wa kijiji cha Vikawe, Kibaha.
Masista
Waabuduo Damu ya Kristo wakielekea meza kuu kwa mwendo wa madaha huku
wakiwa wamebeba zawadi kwa ajili ya kumkabidhi mgeni rasmi na wafadhili
waliojitolea kujenga Zahanati hiyo.
Aliahidi
ushirikiano wa serikali katika kufanikisha usajili wa zahanati hiyo na
kuendelea kuisaidia hatua kwa hatua hadi inakuwa kituo mpaka
watakapofanikisha safari yao ya kuwa hospitali kubwa ya kisasa.
Mganga
huyo pamoja na kutoa ahadi hiyo aliwataka wananchi wa Vikawe kutumia
huduma hiyo na kwamba zahanati hiyo itakapohitaji msaada wa gari la
kubebea wagonjwa (Ambulance) wataletewa kuchukua mgonjwa na kumfikisha
panapohusika.
Zahanati hiyo ya DA.MA Africa imejengwa kwa ufadhili wa wakristo wa Italia chini ya usimamizi wa Muitalia, Germano Frioni.
Akitoa
salamu zake Muitalia huyo amesema kwamba anawashukuru wakazi wa Vikawe
kwa kumpa nguvu ya kusonga mbele hasa kwa kutambua kwamba yeye na
marafiki zake wamefanyakazi usiku na mchana kutafuta fedha kwa ajili ya
kusaidia marafiki wa Afrika.
Alisema atajitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha changamoto za zahanati hiyo zinafanyiwa kazi.
Aliwaomba
wananchi wa Tanzania kuendelea kumuombea yeye na wenzake kama Papa
Francis anavyoagiza ili malengo ya safari ya kuwapo duniani yafanikiwe.
Alisema
kwamba watoto wake Daniel na Marco (kwa sasa wote ni marehemu) ambao
ndio kifupi cha zahanati hiyo DA.MA wamemfanya kujitambua na kusaidia
wengine katika kuonesha upendo.
Aidha
alisema kwamba ataendelea kukumbuka Vikawe kwani alifika mara ya kwanza
mwaka 2005 na kuona hali ilivyokuwa ambapo sasa lipo jengo la zahanati
hiyo likiwa limekamilika.
Wazo
la ujenzi wa zahanati hiyo , lilitolewa na wananchi wa Vikawe kwa
Masisita Waabuduo Damu ya Kristo mwaka 2004 wakati wakiwa katika eneo
hilo baada ya kununua ekari 40 kwa ajili ya kilimo mwaka 1994.
Alisema
pamoja na maombi hayo na wao wenyewe kutambua kwamba kuna mahitaji
makubwa ya huduma ya afya japokuwa kuna zahanati ya serikali, hawakuweza
kutekeleza maombi ya wanavijiji hadi mwaka 2011 walipofanikiwa kupata
ufadhili kutoka Italia na kuanza ujenzi mwaka 2013.
Katika
risala yao walisema kwa ushirikiano kati yao na wafadhili hao
wamefanikiwa kuwapo kwa zahanati hiyo yenye mahitaji yote ya msingi kwa
mujibu wa taratibu za serikali na kuzidi.
Msoma risala alisema kwamba wataendelea kupanua miundombinu mpaka zahanati hiyo ifikie ngazi ya cha afya na baadae hospitali.
Pamoja na ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa masisita hao wameanzisha shule ya awali kuwaandaa wanafunzi wa darasa la kwanza.
Wamesema
kwamba wanaamini kwamba wataendelea kushirikiana na wananchi na wadau
wengine wa afya katika kuimarisha huduma za hospitali hiyo.
Zahanati
hiyo pamoja na vifaa tiba pia ina raslimali ya visima vya maji ya mvua
ujazo zenye ujazo wa lita laki moja na kingine lita 49 elfu, wanatumia
umeme wa sola na jenereta .
Walisema kwamba wanachangamoto ya kukosa umeme wa Tanesco, barabara nzuri na nyumba za wafanyakazi.
Mwenyekiti wa kijiji cha Vikawe, Kibaha, Shabaan Mgini akiwasalimia wageni waalikwa wakati wa utambulisho.
Sr. Theresia Rogatus akisoma risala katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa DMD iliyopo Vikawe, Kibaha.
Mganga
Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi
akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa -DMD
kijiji cha Vikawe, Kibaha. Kutoka kushoto ni Mdau wa Zahanati hiyo, Dr.
Zuberi Mzige wa Hospitali ya Mwananyamala,
Mganga
Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi (kulia)
akimkabidhi zawadi Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa
Italia, Germano Frioni. Anaye shuhudia tukio hilo ni Baba Paroko wa
Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri Bunju...
Mganga
Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akikabidhi
zawadi kwa wadau waliombatana na Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati
hiyo Muitalia, Germano Frioni.
Mganga
Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dr. Happniness Ndosi (wa pili
kulia) pamoja na Mfadhili wa ujenzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa ya
kijiji cha Vikawe, Kibaha, Muitalia, Germano Frioni wakikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Zahanati hiyo inayosimamiwa na Masista
Waabuduo Damu ya Kristo nchini.
Muonekano wa ndani ya Zahanati ya Da. Ma Africa-DMD iliyop Vikawe, Kibaha mkoa wa Pwani.
Mganga
Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dr. Happniness Ndosi akiangalia
chumba cha dawa katika Zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa.
Wageni waalikwa wakijadiliana jambo mara baada ya kufungiliwa rasmi Zahanati hiyo nje ya moja ya chumba cha upasuaji mdogo.
Baba
Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri Bunju akiendesha
ibada takatifu ya misa maalum kabla ya ufunguzi rasmi wa Zahanati hiyo.
Wanakijiji wa Vikawe wakishiriki ibada maalum wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Da. Ma Africa.
Kwaya ikitoa burudani.
Wageni waalikwa na wanakijiji wakishiriki kuimba pamoja na kwaya.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanakijiji na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
Umati wa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe.
Mgeni
rasmi Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness
Ndosi katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wafadhili waliojenga
Zahanati hiyo.
Masista Waabuduo Damu ya Kristo wakifurahia taswira za picha za mnato kutoka kwenye kamera.
Jenereta la Zahanati ya Da.Ma Africa linalotumika kutoa umeme katika Zahanati hiyo.
Muonekano wa nje wa jengo la Zahanati ya Da.Ma Africa kabla ya kuzinduliwa rasmi.
Wanakijiji wa Vikawe na wageni waalikwa wakiingia kukagua Zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni