UEFA SUPER CUP: UKISIKIA MPIRA WA WANAUME NDIO HUU WA BARCELONA NA SEVILLA...


Ukisikia mpira wa wanaume ndio umepigwa usiku huu kati ya Mabingwa wa Ulaya, FC Barcelona na mabingwa wa Europa Ligi, Sevilla.
Timu hizo zimecheza fainali ya Uefa super Cup inayoashiria kufunguliwa rasmi kwa msimu mpya wa Ulaya.
Barcelona chini ya kocha Luis Enrique wameshinda 5-4 katika mchezo uliopigwa kwa dakika 120.
Lionel Messi stole the show early on in Tbilisi after netting two superb free-kicks in the first half at the Dinamo Arena
Dakika 90 zilimalizika kwa sare ya 4-4 ambapo magoli ya Barca yalifungwa na Lionel Messi (6, 16), Rafinha (42), Luis Suarez (54), huku ya Sevilla yakitiwa kambani na Ever Banega (3), Jose Antonio Reyes (57), Kevin Gameiro (72 penalti) na Yevheniy Konoplyanka (81).(VICTOR)
Dakika 30 za nyongeza wazee hao wa kazi waliendelea kutunishiana msuli, lakini Pedro Rodriguez alimaliza kazi dakika ya 115 baada ya kuandika goli la tano na la ushindi.
Barcelona wameanza msimu vizuri kwa kutwaa kombe lao la kwanza.
Manchester United target Pedro scored the winner for Barcelona as they beat Sevilla to win the UEFA Super Cup on Tuesday night
Pedro amefunga goli hilo muhimu wakati huu akiwa katika rada za Manchester United na baada ya mechi hii aliripotiwa kutimkia Old Trafford.
Sevilla's Vitolo chases Barcelona right back Dani Alves as Jose Antonio Reyes (right) and Gerard Pique (left) watch on
Msimu uliopita walitwaa makombe matatu (Treble) kwa maana ya La Liga, kombe la Mfalme na Uefa Champions Leagu.
Je, msimu huu watarudi rekodi hiyo?
Wachezaji wa Barcelona wakisherehekea na taji lao na Super Cup ya UEFA walilotwaa jana baada ya kuifunga mabao 5-4 mjini Tbilisi. Barca walimaliza msimu uliopita wakishinda mataji matatu, Ligi ya Mabingwa, Kombe la Mfalme na La Liga na wanafungua msimu vyema kwa taji la kwanza, Super Cup ya Ulaya.
The Spanish winger was on the edge of the celebrations (right) as Andres Iniesta lifted the trophy above his head
Wachezaji wa Barcelona wakishangilia taji lao la Super Cup ya UEFA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni