BAADHI
 ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamelazimika 
kuuzuia msafara wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais leo alipokuwa 
njiani akitokea Wilaya ya Same kuelekea Wilayani Mwanga mkoani 
Kilimanjaro huku wakimuomba awasalimu na kuzungumza nao, kabla ya 
kuendelea na safari yake.
Bi.
 Samia Suluhu alilazimika kuusimamisha msafara wake baada ya wananchi 
hao kusogea zaidi barabarani wakati akipita huku wakinyoosha mikono ya 
kumuomba asimame ili azungumze nao eneo la kilometa chache kabla ya 
kuingia njia panda. Wananchi hao wengi wakiwa wakinamama walimsimamisha 
kwa kuingia pembezoni mwa barabara alipokuwa akipita na hivyo kulazimika
 kusimama kwa dakika chache na kuzungumza nao.
Akizungumza
 aliwaambia amefarijika na kuwaona na mapenzi makubwa na chama chao 
hivyo kuwaeleza kuwa yeye ni mwanamke pia na anajua kwa karibu kero 
ambazo wanakabiliana nazo akinamama sehemu mbalimbali na kuahidi endapo 
watapata ridhaa pamoja na Dk. John Magufuli atahakikisha anasimamia 
vizuri utaratibu wa kuwawezesha akinamama kupitia vikundi vya kijamii 
ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na familia zao.
Alisema
 yeye ni mwanamke mzazi anatambua shida wanazokumbana nazo akinamama 
hasa kwenye wodi za wazazi hivyo akifanikiwa kuingia madarakani 
atahakikisha anasimamia ipasavyo ilani ya chama ambayo imeeleza vizuri 
juu ya uboreshaji huduma za afya ikiwemo wodi za akinamama na hali ya 
upatikanaji madawa.
"...Matatizo
 ya wanawake nayafahamu vizuri wala sisimuliwi maana na mimi ni mzazi 
nimeingia wodi ya wazazi mkitupa ridhaa na mwenzangu (mgombea urais, Dk.
 Magufuli) nitahakikisha nayasimamia haya vizuri," alisema Bi. Suluhu 
akizungumza muda mfupi na wananchi waliomzuia barabarani wakiomba 
awasalimu.
Alisema
 kero ya maji imekuwa inawatesa akinamama kwa kutumia muda mwingi 
kutafuta maji na kushindwa kuzalisha uchumi wa familia ipasavyo, hivyo 
Serikali ya CCM imeanza mradi wa kutoa maji katika Bwawa la Nyumba ya 
Mungu na kuyaingiza katika vijiji vyenye shida ya maji.
Aidha
 akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara Mwanga ameisikia kero ya 
uhaba wa mabweni kwa wanafunzi wa kike suala ambalo linachangia kwa 
kiasi kikubwa mabinti hao kutiwa mimba na kukatisha masomo eneo hilo na 
kudai suala hilo lipo katika ilani ya CCM mwaka huu na litashughulikiwa 
vizuri endapo watapewa ridhaa na wananchi, ikiwa ni pamoja na suala zima
 la kupambana na kuongeza fursa za vijana ili kukabiliana na uhaba wa 
ajira.
Alisema
 Serikali iliyopita imejitahidi kuongeza huduma za umeme katika vijiji 
ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi lakini katika awamu hii CCM ikipewa 
ridhaa itahakikisha vijiji vilivyobaki kwa baadhi ya maeneo vinawekewa 
umeme. Alisema anawapa akinamama kazi kuhakikisha Dk. Magufuli na 
wagombea wa CCM eneo hilo wanashinda kwa asilimia 80 kwani wao ndio 
wenye ushawishi mkubwa katika familia. Vivyo hivyo kuwataka madiwani 
wanaogombea kuhakikisha mgombea uraisi na wengine wanapata kura za 
kutosha ili kushinda uchaguzi.
Kwa upande wake 
Asumta Mshana aliyekuwa mbunge wa CCM na uchaguzi huu aligombea na kura 
hazikutosha alisema anawashangaa wanachama ambao waligombea ndani ya 
Chama Cha Mapinduzi na waliposhindwa wakaamua kuondoka ndani ya chama 
hicho. 
Alihoji kwani walipokuwa wakiomba nafasi hizo hawakutambua kuna 
kushindwa na kushinda? Aliwafananisha wanaofanya hivyo ni sawa na 
akinababa wanaoamua kukimbia familia zao jambo ambalo ni aibu.
"Nawashauri
 wababi ndani ya chama na kukijenga chama ili kiweze kufanya vizuri, 
kama kura hazikutosha safari hii usikimbie chama kwani mlikuwa hamjui 
kuna kushinda na kushindwa unapoomba uongozi," alisema.
Naye
 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa Idd Juma Mohamed alimshukuru Bi. Samia kwa 
kuamua kuanza kampeni katika mkoa wake na kumuhakikishia watahimiza 
wapiga kura kwani Kilimanjaro bado ni ngome ya CCm na watahakikisha 
wanatwaa majimbo yote, viti vya udiwani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni