NMB DHAMININI MICHEZO YOTE HAPA NCHINI KUONDOA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA

Mahmoud Ahmad Arusha
Raisi wa chama cha riadha hapa nchini na dc wa hai Anthon Mtaka ameitaka taasisi ya fedha ya NMB kuangalia uwezekano wa kudhamini michezo mbalimbali hapa hapa nchini  ikiwemo mpira wa mikono,Mpira wa pete,Ngumi,Kuogelea na riadha ilikukuza michezo hiyo iwe na ushindani na kuitoa nchi kimasomaso kwani michezo kwa sasa ni ajira kubwa kwa vijana.

Kauli hiyo ameitoa wakati akihojiwa na waandishi wa habari kwenye mkutano mkuu wan ne wa wadau wa mfuko wa barabara unaondelea jijini hapa na kusema kuwa kama benki hiyo imeweza kuidhamini timu kama ya Azam na timu ya taifa sasa imefika wakati wa kudhamini michezo mingine.

Mtaka alisema kuwa michezo hivi sasa ni ajira hivyo kama wadau mbali mbali watawekeza katika michezo itapunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana hapa nchini na kulifanya taifa kukua katika michezo na hatimaye kulitangaza kimataifa kupitia michezo mbali mbali.

‘’Imefika wakati NMB mkangalia udhamini wenu katika makundi mbali mbali ya michezo hapa nchini badala ya sasa kuangalia mchezo mmoja pekee wa mpira wa miguu huku nchi ikiendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu katika michezo mbali mbali’’alisema dc Mtaka.

Hapa mmeweza kudhamini taasisi mbali mbali kwenye mambo mbali mbali kama mkutano huu wa wadau wa mfuko wa barabara ifike mahali mkadhamini na michezo mbali mbali kuisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni