TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ofisi
ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasikitika
kuwepo kwa taarifa za uzushi ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya
kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari
kuhusu msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Habari
hizi si za kweli na tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa
Mheshimiwa Makamu wa Rais, hausiki na taarifa hizo zilizoenea kwenye
mitandao ya Kijamii na wala hajapanga tukio lolote la kukutana na
waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake
ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Aidha
tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha
taarifa zisizo sahihi kwa maslahi yao waache kufanya hivyo kwa kuwa ni
kosa kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi
na kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyohusika na kutambulika.
Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni