Jumla ya timu 14 kutoka wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha ,zinachuana vikali katika mashindano ya soka kuwania kombe la SETHBENJAMINI aliyekuwa muasisi wa Azimio laArusha ambaye alifariki mwaka 1967.
Timu hizo ni ST.Domingo , Manyata, Duluti,Rafiki, Railway sports club, Maji ya chai, Embaseni,Usa Star,Meru Worrious, Pande za home Chemchem, Magadini ,Waya mkali na Chackyi SC zinachuana vikali katika mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja vya Ngaresero .
Kwa mara ya kwanza mashindano hayo kufanyika ili kuweza kumkumbuka mwasisi huyo ambaye anakumbukwa kama shujaa ,alikuwa akisafiri kutoka Arusha kwa matembezi kuelekea Dar es salaam ambapo alipofika eneo la maji ya chai ,Usa river alizidiwa gafla na kupoteza maisha papo hapo ilikuwa mwezi julai mwaka 1967 , kwa mujibu wa diwani wa kata ya Usa River (CCM) Zubery Simbano.
Simbano alieleza kuwa wameamua kushirikiana na familia ya marehemu ili kuweza kumuenzi katika soka akiwa yeye ni mmoja wa mashujaa ambao inaonekana wamesahaulika ,hivyo wataendelea kumuenzi na kumkumbuka kila mwaka .
“ Mashindano haya yalianzatarehe 22 Julai na tunataraji yatamalizika tarehe 5 septemba mwaka huu ambapo yata hitimishwa na maandamano kutoka mahali alipozikwa muasisi huyo, eneo la Laki tatu kanisani hadi eneo la uwanja wa Ngaresero na maandamano hayo yatahusiha washiriki wote wa mashindano pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) na Viongozi wa serikali.”alisema Simbano.
Mshindi wa kwanza ataweza kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano (500,000/=) pamoja na kikombe lenye thamani ya shilingi laki mbili na medali,huku mshindi wa pili atajipatia seti ya jezi na mipira miwili sambamba na medali,na mshindi wa tatu atapata mipira 3 na medali.
Pia washiriki wote wataweza kujipatia vyeti ,na kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa mfungaji bora, mchezaji bora na timu yenye nidhamu vile vile mwisho wa mashindano kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwamo mbio za baiskeli za km 40 zitakazo anzia katika uwanja wa ngaresero hadi Raundi ya Impala na zitapitia barabara ya Nelson Mandela,kukimbiza kuku, kuvuta kamba .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni