Aliyevalia shati la blue ni Balozi mdogo wa Kenya Tanzania,Boniface Muhia akiondoka katika banda la kampuni ya Simba
Cement mara baada ya kutembelea banda hilo katika viwanja vya nane nane
Themi jijini Arusha ,kushoto ni Mkurugenzi wa Kenya plant helth
inspectorate service Bi.Esther Kimani(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Wananchi
wakipata elimu katika banda la Simba Cement katika maonyesho ya nane
nane ya kandaele ya kaskazini yanayoendelea katika viwanja vya njiro
Themi jijini Arusha
Ugeni kutoka kenya wakiongozwa na Balozi mdogo wa Kenya Tanzania,Boniface Muhia wakipata maelezo katika banda la Simba Cement
Afisa masoko Mkuu wa kampuni ya Simba Cement Leslie Massawe kushoto akitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda lao katika maonyesho ya nane nane
Tafiti
zimeonyesha kuwa baadhi ya watumiaji wa saruji hapa nchini hawafati
viwango vilivyowekwa na hivyo hupelekea kupata bidhaa isiyo bora kwa
watumiaji wa bidhaa hiyo
Hayo yamebainishwa na afisa masoko Mkuu wa kampuni ya
Simba Cement ambao ni watengenezaji wa Saruji ,Leslie Massawe wakati
akitoa elimu kwa wananchi waliotembea banda lao katika maonyesho ya nane
nane ,kanda ya kaskazini jijini Arusha
Massawe alisema kuwa utafiti uliofanywa na kampuni yao ya saruji inaonyesha kuwa baadhi ya wajenzi hawafuati mchanganyiko unaokubalika baina ya saruji,mchanga,kokoto hivyo inapelekea kupata matofali yaliyochini ya kiwango
“Bidhaa
zetu ni matokeo ya utafiti wa kina na uboreshaji makini unaofanywa na
wataalumu wetu kupitia ujuzi wao wenye sifa zinazozingatia viwango vya
ubora wa simenti Tanzania”alisema Massawe
Aidha
alisema kuwa wanautarabu wa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wateja wao
pamoja na wananchi kwa ujumla juu ya matumizi sahihi ya saruji ,katika
ujenzi wa sekta mbalimbali sanjari na uzalishaji wa viwandani hali
itakayosaidia upatikaniji wa ujenzi wa nyumba imara na miundombinu bora
Alitoa
wito kwa wananchi kupata elimu ya matumizi bora ya vifaa vinavyotumika
katika ujenzi kabla ya kuanza ujenzi,huku akiwataka mafundi ujenzi na watengenezaji wa matofali kutenga muda wa kushiriki semina mbalimbali zinazotolewa na kampuni za saruji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni