Waziri 
wa Fedha Saada Mkuya Salum, (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye 
thamani ya shilingi milioni moja, mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa 
PPF, Sara Haule ikiwa ni malipo ya fao la uzazi wakatinwa uzinduzi wa 
bodi mpya ya PPF, sambamba na uzinduzi wa fao hilo la uzazi, Jumanne 
Agosti 25, 2015.
                                              Waziri Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya uzinduzi
 
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akitoa hotuba ya ukaribisho na 
utambulisho nwakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Mfuko, sambamba na 
uzinduzi wa Fao la Uzazi, ambapo wanachama wawili wa Mfuko, Sara Haule 
na Caroline Kiswaga, walilipwa shilingi milioni 1 kila mmoja kama malipo
 ya fao hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah, akitoa hotuba yake
 Waziri 
Saada Mkuya Salum, Mwenyekiti wa Bodi ya PPF, Ramadhan Kijjah, na 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, wakiwa kwenye picha ya 
pamoja na wajumbe wa bodi ya PPF.
 Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za PPF, na Mamenejawaliohudhuria hafla hiyo, 
Mratibu wa Kanda za Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mbaruku, akielezea namna fao hilo lilivyozingatia Mwanachama na Mwenza wake
                                                       Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF
Waziri 
Saada Mkuya akimpongeza Mwanachama wa PPF, Caroline Kiswaga, baada ya 
kumkabidhi shilingi milioni moja ikiwa ni malipo ya fao la uzazi
Mwenyekiti
 wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah, 
(kushoto), akimkabidi kadi mpya ya uanachama wa Mfuko nhuo, Waziri wa 
Fedha, Saada Mkuya SDalum, wakati wa uzinduzi wa bodi na fao la uzazi, 
hafla iliyofanyika makao makuu ya PPF jijini Dar es Salaam, Agosti 25, 
2015.
Waziri Saada Mkuya, (kulia), akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, 
                                             Waziri Mkuya akiteta jambo na Erio wakati wa hafla hiyo
Meneja 
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,  Elihuruma Ngowi, (kulia), 
akifurahia jambo wakati waziri wa fedha Saada Mkuya Salum, (kushoto), 
akimtania Mwanachama wa PPF, Sara Haule, baada ya kupatiwa malipo ya 
shilingi milioni moja kama fao la uzazi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)













Hakuna maoni:
Chapisha Maoni